Moja ya vitu ambavyo huwa tunajifunza ni kutembea maeneo mbali mbali kwa kutumia usafiri tofauti tofauti. Huu ni usafiri ambao nilikuwa sijaupanda tokea mwaka 1994 nilipokuwa natoka Shinyanga naelekea Tabora. Hatimaye nimeweza kusafiri tena kwa gari moshi (treni) mwaka 2012 nikitokea Dar es Salaam kwenda Tabora hakika nimejifunza mengi humu njiani. Moja ambalo nimejifunza ni kwamba usafiri huu kama ni mtalii ambaye huna haraka na safari yako unaweza kujikuta unaufurahia ila si salama kiafya kwa vile kelele za kutosha si vyema kwa mama mjamzito kupanda treni kwa vile anaweza kujifungulia njiani. Nilitoka Dar es Salaam siku ya Jumanne saa 11 jioni na nimefika Tabora siku ya Alhamisi saa 2:30 asbh. Pia tambua unapopanda treni utakutana na hali zote na watu wa aina zote. Asanteni sana.
 Abiria wakichungulia madirishani.
 Abiria wakipanda katika kituo kidogo cha Pugu, ambapo kituo kidogp treni husimama muda wa dakika 2 mpaka 5.


 Kituo cha Pugu.

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: