Bibi Harusi mratajiwa Veronica Stima akiwa amesindikizwa na kaka yake John Stima kuingia katika ukumbi kwa ajili ya sherehe ya kumuaga (Send Off) iliyofanyika ukumbi wa Student's Centre, Tabora. Ambapo Harusi yake ni Jumamosi Septemba 22, 2012.
 Baba na mama yake mzazi Veronica Stima (kutoka kulia) wakicheza nyimbo ya kikabila la Kifipa.
 Wakwe wa bibi harusi mtarajiwa wakiingia ukumbini kwa madaha.
 Bi Harusi mtarajiwa Veronica Stima akiwa na kaka na dada zake waliomsindikiza katika sherehe yake ya send off iliyofanyika ukumbi wa Student's Centre, Tabora.
 Bibi Harusi Mtarajiwa Veronica Stima akimlisha mtarajiwa wake Bw. Allen Mnene
Wachanga nao hawakuwa nyuma kuonyesha umoja wao na ule wimbo wa kushikana mikono.
 Bwana harusi mtarajiwa Allen na mkewe mtarajiwa Veronica Stima wakienda mbele kwa ajili ya utambulisho.
 ...akilishwa keki na mtarajiwa wake
 Bibi harusi mtarajiwa akiaga wazazi wake, kujitayarisha kuungana na mwenzake
 ...hapa bibi harusi mtarajiwa alikuwa akitoa keki kwa mama mkwe wake mtarajiwa huku kaka yake akiwa amemsindikiza.
 
Mzee Prosper Stima ambaye ni baba bibi harusi mtarajiwa akitoa machache.
Mama Catherine Stima ambaye ni mama mazazi wa bibi harusi nae alipata wasaa wa kutoa machache kwa mwanae.
 Kaka mkubwa John Stima akiongea machache kabla ya kumkabidhi dada yake kwa shemeji zake. Alisema, 'Nawakabidhi dada yangu mpendwa, hana hata doa... nawaombeni msije mkanyanyasa'.
 
...mara baada ya kuongea machache kaka mkubwa alikabidhiwa begi la nguo za bibi harusi, tayari kwa maandalizi ya harusi.
 Aha... Bwana na Bibi Cathbert Angelo nao walikuwepo kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa.
Bibi harusi mratajiwa (wapili kutoka kulia) akiwa na dada zake.
 Muda wa kupata show ulifika na mambo yalikuwa kama unavyoyaona mwenyewe.
Picha ya kumbu kumbu kwa wake na watoto wao.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: