Waziri wa Fedha, Willium Mgimwa (kulia) akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki United Bank for Africa (UBA) Tanzania, Daniel Addo kwenye uzinduzi wa kadi ya malipo ya kabla ijulikanayo kama ‘’Africard’’ ambapo Waziri aliisifu taasisi hiyo kwa kutoa huduma nzuri za kifedha. Nyuma kulia ni Mwenyekiti wa Bodi, Jenerali Robert Mboma na Afisa Mtendaji Mkuu kutoka Nigeria, Gabriel Edgal.  
---
Benki ya United Bank of Africa Tanzania Limited imezindua Africard (VISA Prepaid card), ambayo ni kadi yenye malipo kwa fedha za kiTanzania na inayolipiwa kabla na fedha zinaweza kuongezwa mara kwa mara kwa ajili ya shughuli za fedha mbali mbali.

 Akiongea wakati wa uzinduzi ya kadi hiyo hapo Hyatt regency Dar es Salaam – The Kilimanajaro, tarehe 21 Septemba 2012, Mkurugenzi Mkuu wa benki hiyo, Bw. Daniel Addo alisema kwamba uzinduzi huu wa kadi ya  VISA Prepaid iko sambamba na malengo yao yakupanua  huduma zake kwa wanao tumia huduma zakibenki na wale ambao hawatumii huduma hizi zakibenki kwa kuongeza mfumo wa teknolojia na mawasiliano ambayo itawawezesha kutengeza bidhaa na kutoa huduma za hali ya juu.

Kadi ya Africard ambayo imetengenezwa na UBA ni siluisho kwa watu wote pamoja na wateja wetu, pia ina ondoa usumbufu wa kubeba fedha nyingi ambazo ni hatari.
 
Hapo awali, Mwenyekiti wa Bodi wa United bank of Africa Tanzania Limited, General Robert Mboma ( Rtd) na Afisa Mkuu Mtendaji wa United Bank of Africa, bw. Gabrile Edgal alisema kwamba kadi hii inaweza kutumiwa kwa wale wenye akauti na UBA na wale bila akaunti na benki hiyo kwa kufanya shopping, kusafiria na transfa za kibenki na inakubalika kimataifa katika eneo zote zinazokubali VISA.

Ni kadi ya fedha zaki Tanzania na inawekewa hela kabla yakutumiwa na pia unaweza kuiwekea hela. Inakubalika kimataifa popote kwenye mitandao wa VISA na ATM, sehemu zakunulia bidhaa kama supermarket na hata kwenye mtandao wa intaneti. Kadi hii ya Africard ni salama kwani ina namba ya siri na teknolojia mpya inayohakikisha ulinzi’ alisema Bw. Edgal.

Mhe. Dk. William Mgimwa, Waziri wa Fedha – Jamhuri wa Tanzania na mgeni rasmi katika uzinduzi huu alisema wenye kadi hii ya Africard wananufaika na faida zingine ikiwemo kuweza kuweka mpaka milioni 20 kwa siku wakati kuna uwezekano wakutoa mpaka milioni tano katika ATM.

Kuanzishwa kwa bidhaa hii hasa kwa wakati huu ni muafaka kwasababu inasaidia mkakati wetu wakuhama kutoka kwenye fedha taslimu na kwenda kwenye malipo ya mtandao na makusanyo pamoja na vile vile kuwezesha ishirikishwaji yaki fedha kwa ajili ya watu wa kiTanzania
 
Uzinduzi wa kadi hii ni hatua nyingine katika kujenga aina ya miundombinu ya kimataifa na ndiyo hii ambayo nchi yetu inahitaji kwa  maendeleo. Mimi haswa nimeguswa na kwamba mbali na hii kadi kuwa na uwezo wakuweka mpaka milioni 20, inalenga jamii pembezoni ambao hawaweki fedha zao kwenye benki lakini wataweza pia kutumia kadi hii” aliongezea

Afisa Mkuu Mtendaji wa benki hiyo, bw. Imo Etuk alisema “UBA Africard inaazisha kadi ya VISA ya kulipa kabla kutoka UBA! Ni Kadi ya VISA ya kila mtu: Kadi ya benki bila akaunti ya benki! Na nia yetu nikuipeleka katika nchi nzima ya jamhuri ya muungano wa Tanzania”.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: