· Kwa kuanzia, kuwa katika mahusiano ya kimapenzi kuna faida nyingi kwa mwili, watu walio katika mahusiano bora ya mapenzi huishimaisha marefu na kufurahia afya njema kuliko wale wasiokuwa katika mahusiano ya aina hiyo. Faida hii haina pingamizi kwa sababu ya ukweli kwamba watu wanaokuwa katika mahusiano ya karibu wanajijengea hisia na nguvu fulani ambayo huwasaidia kusaidiana na kujaliana wakati wa shida. Siyo tu kwamba watu walioko katika mahusiano ya aina hii wanaishi muda mrefu lakini pia ni kweli kwamba wanakuwa na furaha na wanaridhika na maisha kuliko wale wanaoshindwa kukaa katika mahusiano.

· Pili, kuwa katika mahusiano mazuri ya mapenzi kunasaidia katika mambo mbalimbali ya kimahitaji. Kusaidiana katika mahitaji mbalimbali baina ya wapenzi ni njia nzuri ya kuwa na maendeleo. Watu wawili wanaoshirikiana pamoja mara nyingi watakuwa na maisha mazuri zaidi ya yule anayefanya peke yake. Unapokuwa na mtu karibu wa kusaidiana naye katika mahitaji ni rahisi kupata mafanikio.

· Tatu, Watu walio katika mahusiano mazuri wanapata msaada wa kijamii; kwa maana ya kuwa na mtu karibu ambaye anajali mahitaji yako ya msingi na hisia zako. Kuwa na msaada wa aina hii kuna faida nyingi, mojawapo muhimu ni kuweza kufanya maamuzi ya busara bila kuwa na mtindio wa mawazo na hofu ama mashaka.

· Nne, kuwa na mwenza katika maisha hufanya maisha kuwa ya faraja zaidi. Kuwa na mtu ambaye mnaweza kushirikiana mambo madogo madogo ya maisha kama kuangalia Tv, kutembea, kula pamoja ni muhimu; inaboresha mahusiano na mara nyingi watu walio katika mahusiano ya aina hii wamekuwa na maisha bora zaidi.

· Tano, Mahusiano ni muhimu kwa sababu wapenzi wana kawaida ya kuangaliana tabia zao hasa zile ambazo ni haribifu, na wamekuwa na kawaida ya kuonyana ama kushauriana kuacha kufanya mambo mabaya na tabia mbaya. Kwa mfano watu walio katika mahusiano ya karibu wamekuwa na tabia ya kujaribu kuwashauri wapenzi wao kuacha kuvuta sigara, kupunguza pombe, kuacha kutumia madawa ya kulevya nk.

· Mwisho, Watu walio katika mahusiano bora ya kimapenzi wanafanya mapenzi mara nyingi zaidi kuliko wale walio pekee. Kufanya mapenzi mara kwa mara, kimpangilio ni muhimu kwa afya bora ya mwili na akili. *Ni muhimu kuzingatia kwamba kufanya huko mapenzi ambako ni bora kwa afya ya mwili siyo kubadilisha wanaume ama wanawake, ila ni kwa mwenza wako ama mke au mume na katika hali ya maelewano, uhuru na amani lakini pia kwa utaratibu unaostahili ndiyo upelekea kuleta faida hiyo.
Baada ya kusema yote hayo, ni ukweli kwamba mahusiano mazuri baina ya wapenzi huwa na faida nyingi kwa watu wenye bahati ya kupata mtu wa kumpenda na hatimaye nao kupendwa pia.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: