Steji ilipambwa hivi. Twanga Pepeta wakiporomosha burudani katika sherehe hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Global, Eric Shigongo (mbele) akimwongoza mgeni rasmi katika sherehe hiyo, Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja (wa tatu kushoto) kuingia ukumbini. Wengine pichani ni wafanyakazi wa Global, Issa Mnally (wa pili kushoto), Sud Kivea (wa pili kulia) na Makongoro Oging' (wa kwanza kulia).
Wafanyakazi wa Global na wageni waalikwa wakijisevia msosi.
Wahariri wa Championi, John Joseph (kushoto) na Phillip Nkini wakigonga menyu.
Wanamuziki wa Twanga Pepeta nao wakishiriki msosi katika sherehe hiyo.
Mgeni rasmi, William Ngeleja (kulia) na Erick Shigongo nao wakipata msosi.
Musa Mateja (kushoto) akiwa na Shakoor Jongo wakati wa msosi.
Mambo yalikuwa hivi pande hizo.
BAADA YA MENYU ILIKUWA NI VINYWAJI NA BURUDANI
Kulwa Mwaibale (kushoto) akiwa na Issa Mnally.
Makongoro Oging' (kushoto) akipozi na Flowers; Khadija Mngwai na Sophia.
Shakoor Jongo (kushoto) akikamua sambamba na Twanga Pepeta.
Twanga wakizidi kupagawisha.
Walusanga Ndaki akiserebuka sambamba na Luiza Mbutu wa Twanga Pepeta.
Wafanyakazi wa GPL wakifuatilia makamuzi ya Twanga Pepeta.
Ally Mbetu (kushoto) katika pozi na Richard Bukos.
Akina Rihanna nao walikuwepo.
Wafanyakazi wakisakata rhumba.
Kampuni ya Global Publishers and General Enterprises Ltd, wachapishaji wa Magazeti ya Uwazi, Championi, Ijumaa, Risasi, Amani na Ijumaa Wikienda, Jumamosi Machi 17, 2012 ilitimiza miaka 14 ya kuzaliwa ambapo sherehe ya maadhimisho hayo ilifanyika katika Hoteli ya Atrium, iliyopo Afrika Sana, jijini Dar es Salaam. Mgeni rasmi katika sherehe hiyo alikuwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja. Wageni waalikwa pamoja na wafanyakazi wa kampuni hiyo walisherehekea vilivyo siku hiyo huku bendi ya Twanga Pepeta International ikitoa burudani kwa wanafamilia hao wa Global.
Toa Maoni Yako:
0 comments: