Habari zenu wapenzi wasomaji wa Kajunason Blog, napenda kuchukua nafasi hii kuwaletea mahojiano ya Bw. Samweli Tenga katika kipindi cha Njia Panda kinachorushwa na Clouds Fm 88.4 ya jijini Dar es Salaam, mahojiano hayo yalifanyika kwa muda wa wiki tatu mfululizo.
Japokua anadai alikua mwanachama wa FREEMASONS, Samwel alikua anajihusisha na biashara ya dawa za kulevya pia na amekiri kufanya biashara hiyo na baadhi ya viongozi wakubwa wa dini wa Tanzania na hata kukaa nao meza moja, hiyo alama kwenye sikio lake la kulia anasema waliwekewa kwa makusudi ili iwe rahisi kutambulika popote atakapotokea, yani ukimuona tu unajua huyu anauza madawa ya kulevya.
 Alama hii ni kubwa ambayo amepigwa katika mguu wake wa kushoto kumtambulisha kuwa ni mwanachama wa FREEMASON, ni alama kama muhuri ambayo imechora ndani ya mfupa ambapo kwa sasa mguu umekuwa ukimuuma sana mpaka kutaka kufanyiwa uparesheni, nembo hiyo baada ya kupigwa iliambatana na KIAPO ambacho popote atakapokwenda atatambulika, alisema kwa sasa ndio inamsumbua sana kwa sababu chuma kilichotumika kumuwekea kimevunja mfupa, na hii aliifanywa huko Afrika Kusini.
---
Bw. Samweli  Tenga ambaye yeye alikwenda nchini Afrika Kusini lakini alikutana na mauza uza mwengi. Alisema kuwa aliamua kukimbilia na kujiondoa kwenye dini hiyo inayodaiwa kuwa ya kishetani baada ya kutoka gerezani huko Afrika Kusini, walikua wanatumwa kwenda kuua watu kwenye ajali na sehemu nyingine, walipewa hirizi maalum za kuwafanya wasioneane lakini baada ya kuona hayawezi hayo maisha alikimbia lakini mpaka sasa anatafutwa kwa sababu alikuwa ndio anamalizia hatua ya mwisho kuingia kwenye  kutajirishwa kwa mali kama inavyotokea kwa waumini wengine, ila akatoroka na baadae ndio akasikia jamaa aliempeleka kwenye hiyo dini nae ameuwawa baada ya kugundulika kwamba alikuwa anataka kujiondoa.

Fuatilia mahojiano hayo:

Siku ya kwanza... ilikuwa ni tarehe 26/02/2012
Siku ya pili.... ilikuwa ni tarehe 11/03/2012
Siku ya Tatu... ilikuwa ni tarehe 18/03/2012
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

3 comments:

  1. Asante sana Kajuna blog kwa kazi nzuri endelea hivi kutupa habari tulio mbali.Mungu akubariki, nimejifunza mengi.
    Mdau
    Sweden

    ReplyDelete
  2. hii habari mbona sioni kitufe cha kuplay ili nisikilize ?

    ReplyDelete
  3. hizi audio mlisha delete ? mbona hazipatikani tena ?

    ReplyDelete