Hapa vijana wakijaribu kulitoa gari ya RAV 4 yenye no T227AKL lililokuwa limetumbukia kwenye mtaro wa kona ya kuelekea mikocheni jijini Dar es Salaam lilipokuwa limegongana na gari nyingine.
 Juhudi za kuokoa gari hoyo zikiendelea.
 Aha! hapa waliamua kuliachia na kuzama kabisa japo juhudi za kuendelea kulinasua kutoka mtaroni ziliandelea. Pia ni vyema wananchi mkaangalia watu makini wa kunasua gari pindi linapopata tatizo maana wengine huongeza matatizo zaidi.
 Aha! haikuwa kazi ya mchezo kulitoa mtaroni.
Gari hiyo aina ya RAV 4 ya kijani ndiyo iliyogongwa na kufanya nyingine kutumbukia mtaroni.
Hapa ni majadiliano ya hapa na pale yaliendelea kati ya mgongwa na aliyemgonga (huyu mwana mama aliyekunja sura) kiulweli mama huyo alikuwa amelewa chakali kiachi cha kumfanya kila mara aombe msamaha jambo ambalo lilimsikitisha askari na asijue la kufanya. Ni vyema madereva mkawa makini wakati wa weekendi. Japo kuna msemo unaosema, "Don't drink and Drive" hata kama bar wameweka parking.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: