Japokua anadai alikua mwanachama wa FREEMASONS, Samwel alikua anajihusisha na biashara ya dawa za kulevya pia na amekiri kufanya biashara hiyo na baadhi ya viongozi wakubwa wa dini wa Tanzania na hata kukaa nao meza moja, hiyo alama kwenye sikio lake la kulia anasema waliwekewa kwa makusudi ili iwe rahisi kutambulika popote atakapotokea, yani ukimuona tu unajua huyu anauza madawa ya kulevya.
 Alama hii ni kubwa ambayo amepigwa katika mguu wake wa kushoto kumtambulisha kuwa ni mwanachama wa FREEMASON, ni alama kama muhuri ambayo imechora ndani ya mfupa ambapo kwa sasa mguu umekuwa ukimuuma sana mpaka kutaka kufanyiwa uparesheni, nembo hiyo baada ya kupigwa iliambatana na KIAPO ambacho popote atakapokwenda atatambulika, alisema kwa sasa ndio inamsumbua sana kwa sababu chuma kilichotumika kumuwekea kimevunja mfupa, na hii aliifanywa huko Afrika Kusini.

Katika moja ya habari ambazo zilisisimua katika kipindi cha njia panda ya redio Clouds Fm ya jijini Dar es Salaam ni habari ya Bw. Samweli Maro ambaye yeye alikwenda nchini Afrika Kusini lakini alikutana na mauza uza mwengi.

Bwana Samwel alisema kuwa aliamua kukimbilia na kujiondoa kwenye dini hiyo inayodaiwa kuwa ya kishetani baada ya kutoka gerezani huko Afrika Kusini, walikua wanatumwa kwenda kuua watu kwenye ajali na sehemu nyingine, walipewa hirizi maalum za kuwafanya wasioneane lakini baada ya kuona hayawezi hayo maisha alikimbia lakini mpaka sasa anatafutwa kwa sababu alikuwa ndio anamalizia hatua ya mwisho kuingia kwenye  kutajirishwa kwa mali kama inavyotokea kwa waumini wengine, ila akatoroka na baadae ndio akasikia jamaa aliempeleka kwenye hiyo dini nae ameuwawa baada ya kugundulika kwamba alikuwa anataka kujiondoa.

Samwel anasema amewahi kwenda kwenye kanisa la FREEMASON hapa jijini Dar es salaam maeneo ya Posta mara moja tu na kukutana na watu kadhaa maarufu wabongo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

3 comments:

  1. Jamani tujuzeni vizuri hiyo njia panda hatukuisikiliza

    ReplyDelete
  2. Nitawawekea mazungumzo hayo ili kwa wale ambao walimiss wasikilize.

    ReplyDelete
  3. Ni vema kaka Cathbert utuwekee hayo mazungumzo, wengine tuko nje ta Tanzania.Hongera kwa kazi nzuri.
    Mdau
    Sweden

    ReplyDelete