Mkurugenzi wa huduma kwa wateja wa kampuni ya simu ya mikononi  ya Airtel Bi. Adriana Lyamba  akizungumza na wanafunzi  wa sekondari ya Canossa  iliyopo Tegeta jijini Dar-es-salaam wakati wa uzinduzi wa programu  mpya ya kuwawezesha wasichana wa shule za sekondari kuweza kujiamini na kufanya maamuzi sahihi yatakayowafaa katika kutimiza malengo yao ya baadae na  jinsi ya   kufikia malengo yao.
 Wanafunzi wa shule ya  sekondari  Canossa   iliyopo Tegeta jijini Dar-es-salaamani wakionyesha ushirikiano kwa kunyoosha mkono ikiwa ni moja ya utaratibu uliotumika ili kuchaguliwa kujibu swali wakati wa mada maalum iliyotolewa na Mkurugenzi wa Airtel huduma kwa wateja bi Adriana Lyamba wakati wa semina maalum kwa wanafunzi hao yenye  lengo la kuwawezesha wasichana kujiamini na kuwa na mbinu za kufikia malengo yao.
 Meneja Huduma kwa jamii wa Airtel Bi.Tunu Kivishe akifuatiwa na  Sigfrida  Mombo mwanafunzi wa kidato cha tatu na  Janeth Jareth mwanafunzi wa kidato cha pili.

Mbele kabisa ni baadhi ya viongozi wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kutoka kulia ni Meneja Huduma kwa jamii Bi. Tunu Kavisheakifuatiwa na Afisa masoko bi. Maria Kimario, Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja Bi.Adriana Lyamba na Meneja Uhusiano Bw.Jackson Mmbando  wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Canossa iliyopo Tegeta ya jijini Dar-es-Salaam salaam wakati wa uzinduzi wa programu  mpya   ya kuwawezesha wasichana wa shule za sekondari  kuweza kujiamini nakutimiza malengo yao ya baadae.
---
*Kumwelimisha mwanamke ni kuielimisha jamii nzima Airtel


Kampuni ya simu za mikononi ya Airtel Tanzania kupitia kitengo cha huduma Kwa jamii imezindua programu ya uwezeshaji kwa wasichana itakayo wawezesha wasichana wenye umri kati ya miaka 14 mpaka 18 katika harakati za kufanikisha malengo yao ya baadae na kuwajengea uwezo wa kujiamini huku mafunzo hayo yakiwa yamebeba ujembe usemao “jenga maisha yako ya  baadae”

Akiongea wakati wa  ufunguzi wa Programu hiyo iliyofanyika shule ya sekondari ya wasichana  Canossa iliyopo Tegeta jijini Dar-es-Salaam Meneja Huduma kwa jamii Bi Tunu Kavishe alisema “Programu yetu inalenga  kuwawezesha wasichana wote walioko shule za sekondari ikiwa ni muendelezo wa dhamira ‘Airtel Shule yetu’ ya kutoa elimu kwa jamii hasa wasichana ili kuendeleza mahusiano yetu mazuri kati ya kampuni
na wateja wetu waaaminifu.

Mbali na hayo ni ukweli kwamba wasichana wanahitaji sana uelewa wa kutosha pamoja na kutimiza malengo ili kuendelea kufanya vizuri zaidi kitaifa au katika ramani ya dunia, Airtel inaamini wasichana hawa wanahitaji nafasi zaidi, mbali na masomo wanayosoma  wanatakiwa kujifunza mbinu mpya za maendeleo kutoka kwa wasichana wenzao na wakubwa ambao wamewazidi umri pia.

Nae,Mkurugenzi wa huduma kwa wateja wa Kampuni ya Airtel Bi.Adriana Lyamba  ambae ndie aliyekuwa mtoa mada katika ufunguzi wa program hiyo kwa mara ya kwanza alisema  “najisikia fahari sana kwa Airtel kunipa nafasi ya kuwa mtoa mada wa kwanza mara baada ya ufunguzi wa program hii ya kuwawezesha wanawake wenzangu katika shule za  sekondari ya wasichana ya Canossa.

Naiomba Airtel kuhakikisha programu hii itaendelea kwa shule nyingine za wasichana Tanzania na igusie mitaala mbali mbali ya uendelezaji wa taaluma kwa wasichana kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kujiamini na kufanya maamuzi sahihi katika maisha. 

Tutawaomba wafanyakazi wengine wa Airtel pamoja na wadau wetu katika biashara kujumuika nasi ili kuwaongezea na kuwapa wanafunzi uzoefu na mbinu mbalimbali  kwa kufanya hivyo itawaweze kuelewa ni jinsi gani wataweza kuchagua na kuendeleza taaaluma bora kwa maisha yao”.

“Kuna msemo unaosema kuwa ‘kumwelimisha mwanamke ni kuielimisha jamii nzima’ kwahiyo tunaamini elimu mtakayotoa sasa  itakuwa chachu ya maendeleo kwa vizazi vijavyo” aliongeza Bi Adriana 

Tumejidhatiti kuisaidia jamii ya kitanzania,mbali na programu hii ya kuwawezesha wasichana  tumekuwa tukisaidia sekta ya elimu kupitia programu ya Shule Yetu kwa kugawa vitabu katika shule za sekondari nchini na nia yetu ni kuendeleza kiwango cha elimu kwa kuwezesha upatikanaji wa vitabu kwa urahisi zaidi kwa wanafunzai wa shule ya sekondari. Tangu tulipoanza hii programu ya kusadia vitabu katika shule ya sekondari kwa miaka saba iliyopita  tumeweza kuwafikia zaidi ya sekondari 800 ambazo zipo nchi nzima.

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: