Wazazi, Walezio na Wananchi wa maeneo mbalimbali Visiwani Zanzibar, wametakiwa kuwafichua wale wote wanaojuhusisha na mtandao wa biashara haramu wa dawa za kulevya hata kama ni watoto wao ili wachukuliwe hatua za sheria.

Afisa Habari wa Jeshi la Polisi zanzbar Inspekta Mohammed Mhina, alisema kuwa wito huo umetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar ACP Aziz Juma Mohammed, wakati akizungumza na wananchi wa shehia za Mkele alipokuwa akitoa elimu juu ya Utii wa Sheria bila Shuruti.

Katika mkutano huo, Kamanda Aziz alisema endapo kila mmoja wetu atatii sheria za nchi bila ya kushurutishwa na kushiriki katika kutenda maovu na kutoa taarifa za wahusika wa dawa za kulevya ni wazi kuwa tatizo hilo miongoni mwa vijana hapa nchini linaweza kupungua au kumalizika kabisa.

Amesema pasipo kutii sheria ni wazi kuwa mbali ya wafanyabiashara wanaoingiza na kusambaza dawa hizo kila mtumiaji anayetumia dawa hizo, nyuma yake kuna kundi kubwa la watu wanaoathirika kwa njia ama nyingine.

Katika mkutano huo baadhi wananchi wakiwemo vijana ambao ndio kundi kubwa la waathirika wa dawa na vitendo vingine vya kihalifu, wameelezea umuhimu wa Ulinzi Shirikishi na Polisi Jamii katika kusaidia kukomesha vitendo hivyo.

Hata hivyo wananchi hao walisema katika eneo la Mkele pamoja na maeneo jirani, wananchi wamejitahidi kuwakemea na hata kuwatolea taarifa Polisi watumiaji wa dawa za kuilevya na wizi wa mali za watu.

Wakiongozwa na Kamishna wa Polisi Zanzibar CP Mussa Ali Mussa, hivi sasa Kila Kamanda wa Polisi katika mikoa ya Zanzibar anafanya juhudi za kuwaelimisha wananchi juu ya utii wa Sheria bila kushurutishwa ili kuepuka kutenda makosa pasipo kujua.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: