Binti Mary Protas (22) mkazi wa mtaa wa Kagera wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam akiwa na mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miezi miwili na nusu baada ya binti huyo na mwanae kutelelezwa na mfanyabiashara wa kukodisha mikanda mjini Iringa
---
Binti Mary Protas (22) mkazi wa mtaa wa Kagera wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam amejikuta akiishi maisha ya kuomba omba katika manispaa ya Iringa baada ya kudaiwa kutelekezwa na mzazi mwenzeke ambae ni mfanyabiashara wa kukodisha mikanda katika manispaa ya Iringa.

Akizungumza na mtandao wa www.francisgodwin.blogspot.com binti huyo alisema kuwa kwa mara ya kwanza alikutana na mfanyabiashara huyo wa kukodisha mikanda jijini Dar es salaam wakati yeye akiwa katika kazi ya kuuza chakula katika moja kati ya Hoteli jijini Dar es Salaam.

Alisema kuwa makubaliano yao yalikuwa ni kuja kuishi kama mke na mume na hivyo kutokana na ahadi hiyo ya kuja kuoana walikubaliana kuzaa mtoto ila baada ya kufanikiwa kumjaza mimba kijana huyo mfanyabiashara alikata mawaliliano hadi alipoamua kumfuata mjini Iringa.

Hata hivyo baada ya kufika mjini Iringa alifukuzwa na mfanyabiashara huyo akihofu mke wake wa ndoa kuja kumfumania .

Alisema kuwa siku alipofika kwa mara ya kwanza mjini Iringa baada ya kufukuzwa kwao Dar es Salaam na familia yake hadi atakapomfuata aliyempa mimba huyo kijana huyo aligeuka mbongo na kumfukuza nyumbani na hivyo kuhifadhiwa na waziri huyo wa burudani chuo cha Ruco .

Hivyo alisema kuwa hadi sasa suala hilo limefikishwa polisi Iringa pamoja na ustawi wa jamii na kusubiri kijana huyo kuitwa.

Kwa sasa ameomba wasamaria wema kumsaidia kupata mtaji na sehemu ya kuishi kwa muda wote atakaokuwepo mjini Iringa ,waweza kuwasiliana na binti huyo kwa ushauri na msaada kwa namba 0755 885218 ama waweza kuwasiliana na mkurugenzi wa mtandao wa www.francisgodwin.blogspot.com kwa namba 0754 026299/0712 750199
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: