HATIMAYE
Kampuni ya Simon Group imeanza mikakati ya kulifufua Shirika la
Usafiri Dar es Salaam (UDA) baada ya kununua mabasi 30 yenye uwezo wa
kubeba abiria 40 kwa lengo la kuboresha sekta ya usafirishaji jijini
Dar es Salaam .
Hii
itakuwa mara ya kwanza kwa UDA kununua magari mengi kwa wakati mmoja
tangu kuanzishwa kwa shirika hilo zaidi ya miaka 38 iliyopita.
Mwenyekiti
Mtendaji wa Simon Group, Robert Kisena aliwaambia waandishi wa habari
Dar es Salaam jana kwamba kampuni yake imejizatiti katika kuifufua
UDA kama ilivyoahidi wakati iliponunua hisa za kuliendesha shirika
hilo.
“Tayari
yamewasili nchini ili kusaidia kuboresha hali ya usafiri katika Jiji
la Dar es Salaam. Kwa sasa mabasi hayo yamehifadhiwa kwa ajili kupigwa
nembo ya UDA.”
Hatua
hiyo ya Kampuni ya Simon Group kuagiza mabasi mengi kwa wakati mmoja
ina badili taswira na mitazamo iliyokuwepo kwamba kampuni hiyo ya
Tanzania haina uwezo wa kuweza kuhimili kikamilifu changamoto zilizopo
kwenye sekta ya usafirishaji.
Baadhi
ya Wabunge wa Jiji la Dar es Salaam walipokuwa wakichangia bungeni
mwishoni mwa mwaka jana walieleza wasiwasi kwa kampuni hiyo kuweza
kuliendesha Shirika la UDA kwa ufanisi kwa madai kwamba haina uzoefu
wa masuala ya usafirishaji.
“Kimsingi
ni kwamba kampuni yetu imejizatiti katika kuleta mageuzi makubwa sana
katika sekta ya usafirishaji abiria hapa nchini, tunayo mipango mikubwa
ni suala la kupewa muda wa kutosha na tutaweza kuthibitisha na kuondoa
wasiwasi kwa abiria pamoja na watanzania wenzetu,” alisema Kisena
Kisena
alisema katika kipindi cha miezi sita iliyopita Kampuni ya Simon
Group imeweza kuingiza kati ya Sh. bilioni 2.7 na Sh. bilioni 3 katika
uwekezaji ndani ya UDA.
Alisema
kiasi hicho cha fedha ni zile za kulipa mishahara ya watumishi wa UDA,
kununua vipuli vya magari pamoja na kununua magari mapya ikiwa ni
fedha kutoka kwenye vyanzo vingine vya mapato kutokana na akaunti za
UDA kusitishwa ili kuweka sawa baadhi ya kasoro zilizojitokeza wakati
shirika hilo lilipokuwa chini ya usimamizi wa Bodi ya Wakurugenzi ya
zamani, chini ya uenyekiti wa Idd Simba.
Kisena
alisema anashindwa kuendelea na harakati nyingine za kuwekeza zaidi
katika UDA hasa kutokana na ukiritimba katika kutatua tatizo lililopo.
Lakini mwekezaji anasema kwamba ameambiwa kwamba katika kipindi cha
mwezi mmoja ujao Serikali itakuwa imekamilisha masuala yake.
“Kazi
iliyobaki kwa Serikali ni namna ya kujiondoa ili sasa Simon Group
iweze kuwa na udhibiti wa kampuni pamoja na uendeshaji wake…ninaamini
kazi hiyo itakamilika katika kipindi hicho cha mwezi mmoja ambacho
kinakadiriwa,” alisema Kisena
Anasema
kama kampuni hiyo itakabidhiwa Shirika la UDA analenga kutoa ajira
kwa Watanzania wengi zaidi kutokana na wingi wa mabasi makubwa ya
kubeba abiria jijini Dar es Salaam. “Tunataraji kutoa ajira nyingi
zaidi kwa Watanzania, maana tunao mpango wa kuingiza nchini mabasi
zaidi ya 1,000,” alisema Kisena
Aidha
taratibu za ukaguzi wa mahesabu ya UDA zimeshakamilika na pengine
Serikali inasuburi dokezo hilo ili taratibu nyingine za kumkabidhi
mwekezaji mpya Simon Group ziweze kufuata.
Mapema
mwezi huu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG),
Ludovick Utouh alisema kuwa ripoti hiyo imewasilishwa Makao Makuu ya
Kampuni ya KPMG nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kuihakiki na
kuangalia ubora wa ukaguzi wenyewe ndipo waikabidhi kwake aweze
kuipitia.
Utouh
alisema anatarajia kuipata ripoti hiyo wakati wowote ili aweze
kuipitia na kuiwasilisha serikalini kwa ajili ya hatua zaidi. Alisema
kwamba ripoti hiyo ilitakiwa kuwasilishwa Januari mwishoni, lakini
kinachofanyika sasa ni kuhakiki zaidi ili iwe kwenye kiwango
kinachokubalika.
Utouh
alisema kuwa KPMG ni miongoni mwa kampuni zinazoanya vizuri kwenye
kazi hiyo na kwamba, hakuna mashaka yatakayoweza kujitokeza juu ya
utendaji wa kazi zao, bali kinachotakiwa kufanyika ni kusubiri wakati
wa kuiwasilisha serikalini.
Kabla
ya ubinafsishaji huo, UDA ilikuwa inamilikiwa kwa pamoja kati ya
Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na Serikali Kuu, kupitia Hazina,
wakiwa na jumla ya hisa 15 milioni ambapo kila hisa moja ilikuwa na
thamani ya Sh100.
Kwa
mchanganuo, Halmashauri ya Jiji ilikuwa inamiliki asilimia 51 ya hisa
hizo, huku Hazina ikimiliki asilimia 49. Februari 11, Bodi ya
Wakurugenzi ya UDA, chini ya Idd Simba, ilikutana na uongozi wa Simon
Group ikiongozwa na Mwenyekiti Mtendaji Kisena na kusaini mkataba,
ambao ulithibitisha kwamba UDA ilikuwa imeiuzia Simon hisa milioni 7.8
sawa na asilimia 52.535 ya hisa zote.
Mkataba
huo ungeifanya Simon Group kuwa mwanahisa mkubwa katika umiliki wa UDA
kwa vile Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na Hazina, wangebaki na
hisa milioni 7.7, ambazo ni sawa na asilimia 47.465.
Baada
ya mkataba kusainiwa, kipengele cha kwanza kiliitaka Simon Group
kulipa asilimia 25 ya fedha za ununuzi wa hisa za UDA (Sh bilioni
1.142) ambazo ni sawa na Sh milioni 285.669, ndani ya siku 14, tangu
kusainiwa ili kuufanya mkataba utambulike kisheria, na Simon Group
ililipa fedha hizo siku hiyo hiyo. Habari kwa hisani ya Fullshangwe Blog
Toa Maoni Yako:
0 comments: