Madereva wa Fuso wakazi wa Moshi Mkoa wa Kilimanjaro, Emili Kimario (33) Kulia na John Kisima (28) kushoto wakiwa ndani ya chumba cha wazi cha mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro kufuatia kukumbwa na tuhuma za kuwasafirisha raia 97 wa Ethiopia baada ya kutiwa nguvuni eneo la Melela Januari 19, 2012 wakiwa na raia hao ambapo wote walisomewa mashitaka ya kutenda kosa la kubeba huku wao kuingia nchini kinyume na sheria za nchi.
Wakitelemka katika lori kutoka Kituo Kikuu cha Polisi cha kati kilichopo barabara ya Kitope baada ya kufika Mahakama ya Hakimu mkazi Morogoro.
Wakiwa wamewekwa eneo la bustani ya Mahakama hiyo ili kusubiri kwenda katika chumba cha Mahakama ya Hakimu mkazi Morogoro ili kusikiliza mashitaka yao yanayowakabili. Picha na Juma Mtanda kutoka Morogoro mwandishi wa Kajunason Blog.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: