Kweli nimesikitika sana kuona hali ya kwetu Bukoba bado tuko nyuma mpaka maiti inabebwa kwa pikipiki yaani thamani ya utu inaishia hapo kweli nimesikitika sana. Sasa tufanyeje kwa walio mbali na Bukoba na walioko Bukoba wenyewe tunatakiwa kujikomboa kununua vifaa viwasaidie ndugu zetu walioko vijijini nakumbuka zamani kama unatoka Kyaka pale mlima katoma lazima ukutana na watu wamebeba maiti kwenye baiskeli wanapelekwa vijini kila mtu anaona sioni wakati wa sasa jamani.
Nakumbuka kuna kampuni moja iko Dar es Salaam wanazo Bajaji nzuri zinaweza kubeba maiti, wagonjwa, wamama wajawazito tukiamua tunaweza kufanya harambee kwa ajili ya watu wa Bukoba tukanunua hizo bajiji kama tano tukapeleka kwenye kata ili mwanakijiji anapopatwa na shida kama hii anakodi kijijini na inasaidia hata kwa maendeleo. Kuna kijiji kimoja mtwara wanakijini baada ya kupata shida walichanga wanakijiji wakainunu kwa 10,000,000/= inawasaidia sana na kijiji ndo kilichagua mtu atakayeindesha na kuitengeneza yaani wako sembuse sisi watu kutoka Bukoba tunashindwa nini?
Pikipiki ikiwa mwendo wa kasi huku imebeba mwili wa marehemu. Kwa habari zaidi unaweza kutembelea Bukobawadau Blog


inasikitisha jamani
ReplyDeletedaaaaaaaaaa hii inasikitisha sn kuona utu wa mtu unakuwa hauna thani kiasi hiki.
ReplyDeleteCjawahi ona. kweli inasikitisha.
ReplyDelete