Na Mwandishi wa Kajunason Blog

Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu,  leo imeshindwa kumsomea maelezo ya awali, yaani PH,  aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), David Mattaka na wenzake wawili kutokana na  mawakili wa upande wa utetezi kushindwa kufika mahakamani hapo.

Mataka anakabiliwa na makosa matatu likiwemo kosa la matumizi mabaya ya madaraka kinyume na Sheria na kifungu 31 Na.11 ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa Na.11 ya mwaka 2007.
.
Washtakiwa  wengine  katika kesi hiyo  ni Kaimu Ofisa Mkuu wa Kitengo cha Fedha Elisaph Mathew Ikomba na Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu ya Ndani, William Haji.

Katika shtaka la kwanza linalowahusu washtakiwa wote  kwa pamoja wanadaiwa kuwa walishindwa kutunza kumbukumbu za mawasiliano ya manunuzi waliyokuwa wakifanya na mtoa huduma kinyume na kifungu cha 55 (3), 87 (1) (f) cha Sheria ya Manunuzi ya Umma Na. 21 ya mwaka 2004 na kanuni ya 17(1) ya Sheria ya Manunuzi (Goods, Works, Non-Consultant Services and Disposal of Public Asets by Tender) Regulation, G.N. No.97 of 2005.

Upande wa mashtaka unadai  shtaka la pili ambalo pia linawakabili washtakiwa wote ni la kushindwa kutimiza matakwa ya vifungu vya Sheria ya Manunuzi ya Umma na Kanuni zake kinyume na kifungu cha 87 (1) (f) cha Sheria ya Manunuzi ya umma ya mwaka 2004.

Shtaka la tatu linalo mkabili Mattaka pekee  linahusu  matumuzi mabaya ya madaraka kinyume na kifungu cha 31 cha Sheria ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa ya mwaka 2007

Mara tu baada ya kesi hiyo kuanza, mapema leo asubuhi upande wa mashtaka ukiongozwa na mwendesha mashtaka kutoka TAKUKURU, BENY LINCOLYNE, ulieleza kuwa uko tayari kwa ajili ya  kesi hiyo ambapo hata hivyo hakimu , RITTA TARIMO alilazimika kuiahirisha mpaka Februari 23 mwaka huu baada ya kuona kwamba  mawakili wa utetezi hawakuwemo katika chumba cha mahakama ilikokuwa ikiendeshwa kesi hiyo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: