Na Mwandishi wa Kajunason Blog
Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jana imetoa hati ya kukamatwa kwa wanafunzi watano, wa chuo kikuu cha es Salaam, sehemu ya Mlimani ambao ni miongoni mwa wanafunzi 51 wanaokabiliwa na kesi ya kukusanyika kinyume cha sheria.
Hakimu Waliarwande Lema amechukua hatua hiyo kufuatia ombi la upande wwa mashtaka lililotolewa na Elizabeth Kaganda, aliyeiomba mahakama itoe hati kwa watuhumiwa hao kutokana na kutofika mahakamani hapo bila taarifa yoyote.
Wanafunzi hao ni Baraka Monas, Godfrey Deogratius, Connel Rwagai, Wilbald Eane na Luciana Ismael.
Kwa mara ya kwanza wanafunzi hao walifikishwa mahakamani hapo, Novemba 14, mwaka jana, wakidaiwa kuwa wakiwa katika eneo la Mlimani kwa pamoja walifanya mkusanyiko usio wa halali na kusababisha uvunjifu wa amani katika eneo hilo.
Kesi hiyo itaendelea tena mahakamani hapo Februari 13 mwaka huu.


Toa Maoni Yako:
0 comments: