Hii ni mojawapo ya CD feki ambazo zimekuwa zikiuzwa mitaani na ina mkusanyiko wa nyimbo mbali mbali za wasanii kama uionavyo pichani, haina muhuri wowote wenye nguvu ya kimamlaka ya sheria, hii ina maanisha kwamba kuna Mtu/watu fulani wanaofanya kazi ya kuwaibia wasanii wetu na kuwafanya waendelee kuwa masikini wa kutupwa kila kukicha. Picha ya CD hii nimeipiga maeneo ya Kinondoni jijini Dar es Salaam ambapo nilikutana na kijana (wamachinga) wanaotembeza mitaani. Serikali ni vyema wakaungana na wasanii ili kuwanusuru na janga hili. Wasanii mnajua kuwa kuna hii CD ipo mtaani inauzwa???

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: