Na mwandishi wa Kajunason Blog, Moshi

Jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro limewakamata watu wanne wakiwemo maafisa wawili wa ardhi kwa tuhuma za kutoa hati ya uongo ya eneo la Manyatta Coridor lenye ekari 3131 lililoko wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro.

Akizungumza Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro Absolom Mwakyoma alisema eneo hilo la  Manyatta Coridor lilitengwa na serikali kwa ajili ya ibada ya kabila la wamasai ambapo lilimilikishwa na Wizara ya Maliasili na Utalii chini ya kurugenzi ya mambo ya kale ili lihifadhiwe kwa ajili ya shughuli hizo za kimila.

Kamanda Mwakyoma alisema serikali iliagiza pia eneo hilo lisijengwe nyumba za makazi yoyote isipokuwa malisho ya mifugo.

Kamanda huyo wa Polisi aliwataja waliokamatwa kuwa ni Elizabeth Kundy ambaye ni Afisa ardhi wilaya ya Siha, Christopher Mwamasage ambaye ni Afisa Ardhi kutoka wilaya ya Siha na Hai, Greyson Jacob ambaye ni Mpimaji Ardhi eneo la Sanya Juu na Japhet Samisi ambaye ni Fundi Sanifu mkuu.

Alisema kukamatwa kwa watuhumiwa hao kunafuatia kugunduliwa kwa ujenzi wa kituo cha mafuta cha Kobil Tanzania Limited na kamati ya ulinzi na usalama mnamo Mwezi Juni mwaka jana.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: