Katika hali isiyokuwa ya kawaida mtu moja aliejulikana kwa jina la Juliana Kata Miti mkazi wa Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa amekutwa ameuwawa katika mazingira ya kutatanisha tukio ambalo limevuta hisia tofauti kwa wakazi wa eneo la Kizwite.
Kamanda wa polisi mkoa wa Rukwa Isuto Mantage amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema limetokea majira ya alfajiril eo asubuhi katika eneo la kata ya Kizwite karibu na shule ya Msingi Kizwite Dampo ambapo mwili wa marehemu umekutwa.
Uchunguzi wa awali wa kipolisi unasema kwa mara ya mwisho husiku wa kuamkia siku ya tukio marehemu alikuwa na mume wake wa zamani hadi saa nne usiku alietaka warudiane.
Kamanda Isuto amesema uchunguzi bado unaendelea juu ya tukio hilo.
Toa Maoni Yako:
0 comments: