Hatimae Kampuni ya simu za mikononi ya AIRTEL imekabidhi gari lenye thamani ya shilingi milioni sitini na tano kwa mshindi wa shindano la Jivunie lililofanyika 2010 bwana Immanuel Kapungu mkazi wa Sumbawanga katika kijiji cha Muze.
Akikabidhi zawadi hiyo kwa mshindi huyo mkuu wa wilaya ya Sumbawanga Kanali mstaafu John Mzurikwao amesema kutolewa kwa gari hilo ni changamoto kwa wateja wengine kushiriki mashindano.
Gari hiyo aina ya Toyota Rav 4 inakuwa ni gari ya pili kutolewa mkoani Rukwa huku mshindi mwingine akiwa amekwisha kabidhiwa mwezi wa nane mwaka jana kama anvyoeleza meneja wa biashara wa AIRTEL kanda ya nyanda za juu kusini Fredrick Mwakitwange.
Toa Maoni Yako:
0 comments: