Na mwandishi wa Kajunason Blog
Watu watatu wamekufa kwa kupigwa na risasi kutokana na ugomvi wa kifamilia, katika eneo la Bamba katika halmashauri ya mji wa Kibaha, jana saa mbili na nusu usiku.
Watu watatu wamekufa kwa kupigwa na risasi kutokana na ugomvi wa kifamilia, katika eneo la Bamba katika halmashauri ya mji wa Kibaha, jana saa mbili na nusu usiku.
Akithibitisha habari hizo kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Pwani, Erenest Mangu amethibitisha juu ya kutokea kwa kutokea kwa tukio hilo leo, alipokutana na waandishi wa habari ofisini kwake leo mchana, Ambapo amesema kulikuwa na kikao cha kifamilia kuhusiana na mgogoro wa ardhi ambayo inakadiriwa na ukubwa wa ekari mbili, kati ya wanandugu na kikao hicho kilikuwa kinafanyika nyumbani mwa Mratibu wa TASAF wa mkoa wa Pwani na Dares saalam Bw. Pendael Senge.
Na ndipo mmoja wa wanandugu wa kituo cha Polisi Magomeni Bw. Nicodemus Senge ambaye alikuwa na bastola ambayo aliitumia kuwapiga risasi ndugu zake ambao alikuwa anabishana nao na kuwauwa pale pale kabla ya yeye mwenyewe nae kuamua kujimaliza kwa kujipiga risasi.
Wengine ambao waliuwa katika tukio hilo ni Bw. Andrew Senge mfanyabiashara mkazi wa Kiwalani aliyepigwa risasi ya kichwa na Bw. Nkolo Senge aliyepigwa risasi meneo ya kifuani anayesemekana kuwa alikuwa akifanya kazi katika ofisi ya Bunge.
Toa Maoni Yako:
0 comments: