Mwenyekiti wa Wananchi Group ambao ndio waanzilishi wa ZUKU TV,Ali Mufuruki akizungumza wakati wa uzinduzi wa ZUKU TV uliofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye Hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam.


Mkurugenzi mkuu wa TCRA,John Nkoma akizungumza wakati wa uzinduzi wa ZUKU TV uliofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye Hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Wananchi Group, Ali Mufuruki (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Wananchi,Richard Bell (katikati) wakibadirishana mawazo na mmoja wa wadau wa ZUKU TV wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo uliofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye Hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam.
Baada ya Uzinduzi, sasa ni Utambulisho kwa wadau.
Wadau Mbali Mbali walihudhuria uzinduzi huo.
Wadau.
Mdau Raqey na Mai waifu wake Sarah.
TMK wanaume wakifanya vitu vyao stejini.
Dogo Asley na kundi zima la TMK wakionyesha mambo yao.


Dj Choka.
AY akipagawisha mashabiki wake.
Zuku ilizinduliwa rasmi usiku wa kuamkia jumamosi katika sherehe ya kufana iliyofanyika kwenye ukumbi wa Golden Tulip. Sherehe hii ilihudhuriwa na wajumbe, waingizaji, wajasiriamali na watu mbalimbali walioshuhudia uzinduzi wa Zuku TV.
Mwenyekiti wa Wananchi Group, heshimiwa Ali Mufuruki aliongelea mfumo mzima wa kiufundi wa runinga, ikifuatiwa na maonesho ya fataki na pia burudani toka kwa wasanii mbalimbali kuwadhihirisha wageni wote.
"Tunayo furaha kuzindua TV ya Zuku hapa Tanzania," Alisema Richard Bell, Afisa mkuu mtendaji wa Wananchi Group. "Ni hatua kubwa kwetu na tunafarijika kuweza kutoa burudani bora majumbani kwa watu wote.
Televisheni ya Zuku inatoa uchaguzi mpana wa stesheni za burudani ikiwa ni pamoja na Habari, Michezo na Sinema, majarida na muziki. Hivi vinajumuisha chaneli za nje kama vile BBC, MTV Base, Sentanta Sports, MGM movies na zinginezo nyingi. Pia Msambazaji hutoa ofa kabambe za stesheni kama vile Zuku Afrika ambayo huonesha bara la Afrika, Zuku Maishaambayo huonesha makala mbalimbali, Zuku Michezo pamoja na chaneli lukuki za sinema. Huduma hii ya Zuku hupatikana kupitia satelaiti Tanzania nzima.
Toa Maoni Yako:
0 comments: