Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoa wa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian Masawe amekanusha vikali madai yaliyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini kuwa wanajeshi wa serikali ya Burundi wanapigana na wanajeshi wa nchi hiyo walioasi kwenye ardhi ya Tanzania katika wilaya ya Ngara mkoani humo.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Kanali Masawe ambaye pia ni mkuu wa mkoa wa Kagera amesema kuwa madai hayo hayana ukweli wowote bali kinachotokea katika eneo la mpaka ni kwamba wanajeshi walioasi hukimbilia Tanzania katika wilaya ya Ngara pale wanapozidiwa nguvu na majeshi wa serikali ya Burundi.
Kanali Masawe ameongeza kuwa tayari ulinzi mkali umeimarishwa katika maeneo yote ya mpaka kati ya Tanzania na Burundi Wilayani Ngara ili kudhibiti vitendo vya wanajeshi wa Burundi walioasi kukimbilia nchini pale wanapozidiwa nguvu na majeshi ya serikali.
Toa Maoni Yako:
0 comments: