Askari wakijichukulia sheria mkononi. Hii picha imewekwa hapa kuonyesha jinsi ambavyo raia wamekuwa wakipigwa na Polisi ila haihusiani na tukio la Iringa.
Vijana waliopigwa na FFU Jumanne Hafidh mwenye sweta jekundu na George
Mbilinyi (kulia) wakisubiri matibabu katika hospital ya mkoa wa Iringa
pamoja na ndugu zao.
---
Sakata la askari wa kikosi cha tukuliza ghasia FFU mjini Iringa kupiga raia wasio na makosa limeanza kuchukua sura mpya baada ya wanaharakati na wananchi kutaka jeshi la polisi kuwachukulia hatua askari wake waliohusika huku wakitaka dereva wa gari la FFU kuacha mara moja kuendesha gari hilo kidharula kila wakati kukimbiza gari bila sababu ya msingi.
Wanaharakati hao wameueleza mtandao huu wa http://www.francisgodwin.blogspot.com/ kuwa wanaliomba jeshi la polisi kupitia kamanda wa polisi mkoa RPC Evarist Mangalla kuwawajibisha askari wake kama ambavyo wananchi wakifanya kosa wanavyowajibishwa.
Wakati madereva mjini Iringa wakitaka kikosi cha usalama barabarani kutoa onyo kali kwa madereva wa magari hayo ya FFU ambao kila siku na kila dakika wao wapo katika dharula na kuendesha gari kwa mwendo mkali huku wakitambua wazi kuwa sheria vinapinga mjini kukimbiza gari kwa zaidi ya spidi 100.
Kwani walisema askari hao wa FFU wanatambua wazi kuwa kila siku majira ya saa 6 mchana na saa 12 jioni wanapaswa kwenda lindo katika mabenki hivyo ni vema kuanza safari kabla ya muda huo hata kuanza kuondoka saa moja kabla badala ya kuonekana wapo dharula muda wote na kuleta madhara kwa watumiaji wengine wa barabara.
Wakati huo huo taarifa ambazo mtandao wa http://www.francisgodwin.blogspot.com/ umezipata jeshi la polisi limeanza kutafuta suluhu la vijana wawili waliopigwa na FFU HaFidh Jumanne (26) mkazi wa Ilala na Dereva George Mbilinyi (25) ambao walijeruhiwa na kunyimwa haki yao ya kupewa fomu namba tatu (PF3) kwa ajili ya kwenda kutibiwa ambapo jana wametafutwa na kupewa fomu hiyo kwenda kupatiwa matibabu katika Hospital ya mkoa na kufungua kesi hiyo ya shambulizi toka kwa askari wa FFU.

Shukrani zikuendee; http://www.francisgodwin.blogspot.com/ kwa kuendelea kutuletea habari kutoka Iringa. Kajunason Blog inakupongeza sana kwa juhudi ambazo umekuwa ukizifanya kutetea haki za jamii.
Toa Maoni Yako:
0 comments: