Wakati wa kuadhimisha Miaka 50 ya uhuru wa Tanzania Bara Ubalozi wetu hapa nchini Uingereza wakishirikiana na Chuo kikuu cha mji Coventry wanapenda kuwatangazia wadau wote wa elimu kuwepo kwa Scholarship sita maalum za masomo kwa watanzania ambazo zimetolewa kutoka katika Chuo kikuu cha Coventry katika nyanja zifuatazo:


1. MSc Oil & Gas Management  
    Coventry Campus
    Kuanzia Septemba 2012 

2. MBA Oil & Gas Management
    London Campus
    Kuanzia April, July, Septemba 2012

3. MSc Finance & Investment 

    IAA Dar Campus
    Kuanzia Septemba 2012

4. MBA Logistics 
    IAA Dar Campus
    Kuanzia Septemba 

5. MSc Finance & Investment

    IAA Arusha Campus 
    Kuanzia Septemba 2012

6. MBA Logistics
    IAA Arusha Campus
    Kuanzia Septemba 2012
Jinsi ya kujiandikisha, tembelea tovuti ifuatayo hapo chini:
http://www.coventry.ac.uk/tanzania2012scholarship


Mbali na hapo Ubalozi wetu ukiwakilishwa na Balozi Mh Peter kallaghe, Chabaka Kilumanga na Allen Kuzilwa  walipata fursa pekee ya kukutana na kumpongeza afisa wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Ndg. Semu Mwakyanjala ambaye pia ni mwanafunzi wa shahada ya Pili( Masters Degree in Communication, culture & Media) katika chuo kikuu cha Coventry alieshinda tuzo ya kuandika insha kuelezea jinsi gani nchi ya Ujerumani itakavyokua mwaka 2051.


Aidha Mh. Balozi Kallaghe alimpongeza sana Afisa Semu kwa juhudi zake kwa kufanikiwa kushinda tuzo hii na kuiletea heshima Tanzania Ughaibuni na kuwahamisisha watanzania wote  kusoma na kufanya kazi kwa bidii zaidi. Wakati akiongea na waandishi wa Habari afisa Semu alianza kwa kutoa shukrani kwa familia yake, wafanyakazi wenzake kutoka TCRA na Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania kwa kumwezesha kufikia hatua aliyopiga leo.

kwa maelezo zaidi wasiliana na ubalozi wetu hapa London 00 44 20 7569 1470


Tafadhalini watanzania wote chukueni hii nafasi mapema iwezekanavyo kwa wale wote mnaopenda kujiendeleza kimasomo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: