Wananchi wa Kitongoji cha Makanya kilichopo katika Kijiji cha Mzeri wilayani Handeni katika mkoa wa Tanga, wameanzisha ujenzi wa shule mpya ya Msingi katika kitongoji chao kwa lengo la kupunguza adha kwa watoto wao kusafiri umbali wa kilometa tano kwenda kufuata masomo katika shule ya Msingi Mzeri.
Mwenyekiti wa Serikali ya Kitongoji hicho Bw. Rashidi Mhina na Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Mzeri Bw. Muhaji Mlaki, wamesema kuwa, ujenzi wa shule hiyo mpya unafanywa kwa njia ya Kujitolea.
Wamesema mbali ya wanachi hao kuchangia fedha taslimu ya ununuzi wa vifaa za ujenzi, wananchi hao pia wanachangia nguvu zao katika Kupasua mawe na ukusanyaJI wa mchanga kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa shule hiyo.
Wamesema tayari Mbunge wa jimbo la Handeni Dk. Abdallah Kigoda ametoa msaada wa mabati 60 yatakayoanza kuezeka chumba kimoja cha darasa katika shule hiyo ikilengwa kuanza kuwaandikisha wanafunzi wa darasa la kwanza waanze masomo hapo mwakani na wakaiomba Serikali ya Wilaya kujipanga kupeleka waalimu.
Nao baadhi ya walezi na wazazi wenye watoto katika kitongoji hicho, wamesema kukamilika kwa ujenzi wa shule hiyo kutakua ni ukombozi kwa watoto wao ambao wanapaswa kusafiri umbali wa kilometa kumi kila siku kwenda shule ya Mzeri na kurudi tena Makanya.
Mzee Mwinjuma Rashidi Tilibwinda, amesema pamoja na wao kujitolea kwa michango ya fedha na nguvu zao katika ujenzi wa shule hiyo, pia Kanisa la Pentecost wilayani Handeni, limejitolea kusaidia usombaji wa mawe na mchanga na kujenga vyumba vitano vya madara kwenye shule hiyo ili kusaidia nguvu za wananchi katika ujenzi hao.
Amesema sambamba na ujenzi wa shule hiyo, Kanisa hilo pia limejitolea kujenga Zahanati katika Kitongoji hicho ili kupunguzia adha kwa wagonjwa wakiwemo vikongwe, watoto wadogo na akina mama wajawazito wanaolazimika kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za afya katika kijiji mama cha Mzeri ama makao makuu ya Kata Misima ama wilayani Handeni.
Kwa upande wao, watoto wa kitongoji cha Makanya ambao wanasoma katika shule ya Msingi Mzeri, wamesema wamekuwa wakilazimika kushinda na njaa kila siku kwa kushindwa kurudi majumbani kujipatia chakula cha mchana hata wakati wa mapunziko kutokana na umbali uliopo.
Mbali ya kusafiiri umbali mrefu kutoka katika kitongoji cha Makanya hadi Shuleni Mzeri, lakini pia wanafunzi hao wameelezea mateso wanayoyapata hasa nyakati za mvua ambapo wanalazimika kusafiri hata kama watalowana kwa vile elimu haingoji mtu.
Naye Mjumbe wa Serikali ya Kijiji cha Mzeri Bw. Issa Athumani Mbelwa, amesema kuwa umbali huo umekuwa ukizorotesha mahudhulio ya watoto shuleni kutokana na kuchoka kutembea.
Kwa muda mrefu Kitongozi hicho cha Makanya cha Makanya chenye zaidi ya watoto 400 hakina shule ya msingi na wamekuwa wakitegemea shule ya Msingi Mzeri iliyopo katika kijiji mama.
Hata hivyo, kuna habari pia kuwa, Kitongoji cha Makanya, ni miongoni mwa vitongoji vitatu vya Kata ya Misima vilivyopewa hati ya kuwa vijiji kamili katika Kata hiyo. Vitongoji vingine vilivyopata hati ya kuandikishwa kama vijiji kamili ni Msomela na Mainga ambavyo ambavyo vipo umbali mrefu na huduma za kijamii kama vile shule na Zahanati.

Toa Maoni Yako:
0 comments: