Kila sehemu palikuwa pamejaa maji...
 Mwendesha pikipiki akiwa anatafakari kwa kuangalia maji ambayo yamejaa.
Nyumba zilikuwa zinaelea wenye maji.
 ...wengine walikuwa wakijiokoa wenyewe japo maji yalikuwa ni mengi.
 ...zoezi la kuchota maji lilikuwa likiendelea
 Wengine walikuwa wakitoa vyombo ndani
 ...angalia mto ulivyokuwa umejaa
 ...kila mmoja alikuwa akiangalia ustarabu wa kutoka huku bondeni
 ...wananchi wakijadili namna ya kuwaokoa wenzao na kufikiria pa kwenda baada ya makazi yao kujaa maji kutokana na mvua iliyonyesha usiku wa kuamkia leo.
 ...watoto walikuwa wakichimba mtaro ili kuyaelekeza maji yatoke kwenye makazi yao.
 ...Wengine walikuwa wameshaandaa mahema kwa ajili ya kulala
 ...ndege ya polisi ilikuwa akijaribu kuweka mambo sawa kwa kuangalia usalama wa raia.
Mvua kubwa iliyoanza alfajiri ya leo jijini Dar es Salaam na maeneo mengine nchini, imesababisha  adha kubwa kwa wakazi wa jiji hili ambapo wengi wao walijikuta katika matatizo makubwa baada ya nyumba zao kuzingirwa na kujaa maji. Kajunason Blog ilitembelea maeneo ya Mwananyamala Kisiwani, Kigogo na Tandale na kujionea hali mbaya iliyosababishwa na mafuriko hayo ambapo  baadhi ya watu walilazimika kupanda  juu ya mapaa ya nyumba zao na wengine hawakuthubutu kutoka ndani kabisa kutokana na nyumba zao kuzungukwa na maji.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: