Viongozi wa Klabu ya Simba wametakiwa kuwajibika kutokana na timu hiyo kushindwa kufanya vizuri kwenye baadhi ya mechi za Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara iliyomaliza mzunguko wake wa kwanza jana.
Akizungumza na blog hii, Mweka Hazina wa Simba Tawi la Kibaha Kwamfipa, Fahim Lardhi, alisema kuwa viongozi hao ngazi ya taifa kama wameshindwa kuiongoza klabu hiyo ni vema wakajivua uongozi mapema, ili timu hiyo isivurunde baadhi ya mechi ambazo kwa asilimia kubwa viongozi hao wamekuwa chanzo.
Lardhi alisema kuwa viongozi hao katika msimu wa Ligi Kuu mwaka jana, waliongoza ligi hiyo vizuri na baadaye walianza kuvurunda na hatimaye kuukosa ubingwa.
“Hawa viongozi wa klabu yetu kama wameshindwa kazi waliyopewa na wanachama, ni vema wakajiuzulu mapema kabla hawajasababisha matatizo makubwa, kwani dhahiri wanaonyesha kushindwa kuiongoza klabu na kusababisha timu kuvurunda katika baadhi ya michezo inayocheza,” alisema.
Aliongeza kuwa viongozi hao wameonesha wazi kutokuwa makini katika uongozi wao hivyo kusababisha timu hiyo kuvurunda, kwani mwaka jana waliongoza vizuri na baadaye kushindwa kutwaa ubingwa kwa kukosa pointi moja, hali ambayo inahisiwa kujirudia tena msimu huu.
Aliwataka viongozi hao, kutoingiza mambo ya siasa kwenye michezo ili waweze kuongoza vizuri klabu hiyo na iendelee kutwaa ubingwa katika mashindano mbalimbali.

Toa Maoni Yako:
0 comments: