BAADHI ya wananchi wa Marangu, Wilaya ya Moshi Vijijini, mkoani Kilimanjaro, wamelalamikia kitendo kilichofanywa na Jeshi la Polisi cha kuwazuia kula chakula cha mchana kilichoandaliwa na Mangi wao, Frank Marealle.

Mangi wa Marangu alikuwa ale chakula cha mchana na wana Marangu Oktoba 29, mwaka huu, lakini alipata zuio kutoka mahakamani la kumtaka kusitisha sherehe hiyo, hatua iliyowalazimu polisi kulizunguka eneo la Kibo Hotel ilipokuwa ifanyikie sherehe hiyo.

Mmoja wa wananchi hao, Tumainiel Kimang’ano, alisema kuwa walishangazwa na kitendo hicho cha polisi kuingilia shughuli za kimila ambazo wamekuwa wakizifanya miaka mingi bila kuvunja sheria za nchi.

Naye, Stephano Ndeonaki, kutoka Kijiji cha Mbae, alisema kuwa Mangi aliwakaribisha kwa ajili ya chakula cha mchana na walipofika hotelini hapo walikuta zaidi ya magari manne ya polisi na polisi kuwazuia, jambo alilodai kuwashangaza kwa vile hakukuwa na vurugu.
Mwananchi mwingine, Stephano Agustino, alisema kuwa watu zaidi ya 800 walikuwa wameshajitokeza lakini polisi walifika eneo hilo na kubomoa mahema, kubeba viti na pombe ya kienyeji (mbege), jambo alilodai ni kuingiliwa kwa mila zao za Kichagga.

Kwa upande wake, Mangi Marealle, alisema kuwa ni kweli sherehe hiyo ilizuiwa na polisi kutokana na zuio la Mahakama; lakini tayari chakula na vinywaji vilikuwa vimeshaandaliwa na hivyo kusababisha hasara zaidi ya sh. milioni 20.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: