DAKTARI wa Hospitali ya Wilaya ya Ukerewe, mkoani Mwanza, Andrea Mabula (27), amekutwa amekufa nyumbani kwake katika kifo kilichozua utata.
Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo, Dk. Faustine Nkinga, alisema kuwa marehemu alikutwa amekufa kitandani katika chumba chake majira ya saa moja asubuhi ya Novemba mosi, mwaka huu.
Alisema kuwa majirani zake walitilia shaka baada ya daktari huyo kushindwa kutoka nje asubuhi hiyo kama ilivyo kawaida yake na ndipo walitoa taarifa kwa uongozi wa hospitali hiyo na zikafanyika juhudi za kuvunja mlango.
Alifafanua kuwa siku moja kabla ya tukio hilo, Dk. Mabula alifika kazini na kutekeleza majukumu yake vyema akiwa na afya njema. Kufuatia tukio hilo tayari sampuri za mwili wake zimechukuliwa na kupelekwa kwa mkemia mkuu kwa uchunguzi.
Mashuhuda wa tukio hilo walisema kuwa kabla ya kifo chake, Dk. Mabula alitapika na kutokwa na haja kubwa hali ambayo inadhaniwa kuwa pengine alikula au kunywa kitu chenye sumu.
Naye Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Leberatus Barlow, alisema jeshi hilo kwa kushirikiana na uongozi wa hospitali hiyo, wanaendelea na uchunguzi wa kina ili kubaini sababu za kifo chake.

Toa Maoni Yako:
0 comments: