BENDI ya Extra Bongo ‘Next Level’ inatarajia kuwatambulisha wanamuziki wake wapya kwa mashabiki katika Wilaya za Songea, Mbinga mkoani Ruvuma na Njombe, mkoani Iringa kuanzia Novemba 15 mwaka huu.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa bendi hiyo, Ally Choki, utambulisho huo utawahusu wanamuziki wapya watano na wa zamani ambao ni Super Nyamwela, Rogert Hegga ‘Caterpillar’, Super Danger, Otilia Boniface, Saulo Ferguson na Aisha Madinda.
Choki alisema, utambulisho wa wanamuziki hao unakwenda sambamba na maandalizi ya albamu yake ya kwanza, ambayo amejipanga kuiachia Februari mwakani.
“Extra Bongo, tunakwepa kuzindua albamu wakati wa sikukuu kwa sababu mara nyingi siku kuu hujitokeza watu hata ambao wasio mashabiki wa muziki,” alisema Choki.
Toa Maoni Yako:
0 comments: