Mganga mkuu wa Manispaa ya Temeke, Dr. Sylvia Mamkwe akiwakaribisha wageni waliofika katika hospitali ya Temeke jijini Dar es Salaam, kutoka kulia ni Dr. John Bwana- Kaimu Mganga Mkuu wa Manispaa ya Temeke, Dr. Heavengton Mshiu-MOHSWI RCH (Programe Officer- Safe Motherhood International), Muwakilishi wa Shirika la Mfuko wa Idadi ya Watu la Umoja wa Mataifa (UNFPA)-Tanzania, Dr. Julitta Onabanjo pamoja na Dokta bingwa wa watoto- Temeke hospitali Dr. Solanki Rajeshi.


Pichani juu na chini ni baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria kwenye hafla hiyo.
Muwakilishi wa Shirika la Mfuko wa Idadi ya Watu la Umoja wa Mataifa (UNFPA)-Tanzania, Dr. Julitta Onabanjo akifafanua jambo mapema leo asubuhi wakati hafla fupi ya kutoa msaada wa vifaa mbalimbali kwa hospitali ya Temeke.
Pichani ni baadhi ya misaada mbalimbali iliyotolewa na Shirika la Mfuko wa Idadi ya Watu la Umoja wa Mataifa (UNFPA)-Tanzania kwa hospitali ya Temeke jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la Mfuko wa Idadi ya Watu la Umoja wa Mataifa (UNFPA)-Tanzania waliofika katika halfa ya ugawaji wa misaada katika hospitali ya Temeke jijini Dar es Salaam.
Pichani Muwakilishi wa Shirika la Mfuko wa Idadi ya Watu la Umoja wa Mataifa (UNFPA)-Tanzania, Dr. Julitta Onabanjo akitoa risala na shukarani kwa watu waliofika katika maadhimisho ya watu bilioni 7 Duniani yaliyoendana na utoaji wa misaada kwa hospitali ya Temeke jijini Dar es Salaam iliyofanyika mapema leo asubuhi hospitalini hapo.
Pichani Dr. Husna Msangi ambaye ni mganga wa hospitali ya Temeke akikimkabidhi hotuba kwa mgeni rasmi kwa niaba ya Mganga Mkuu wa TMK hospitali jijini Dar es Salaam, ambaye ni muwakilishi wa UNFPA-Tanzania, Dr Julitta Onabanjo na wageni wengine waalikwa  mbalimbali waliohudhuria (hawapo pichani) kwenye hafla hiyo fupi ya kukabidhi msaada wa vifaa mbalimbali, iliyofanyika mapema leo asubuhi, ambapo Dunia ilikuwa ikitimiza idadi ya watu bilioni 7.
Pichani Dr. Husna Msangi ambaye ni mganga wa hospitali ya Temeke akisoma hotuba kwa mgeni rasmi kwa niaba ya Mganga Mkuu wa TMK hospitali jijini Dar es Salaam, ambaye ni muwakilishi wa UNFPA-Tanzania, Dr Julitta Onabanjo na wageni wengine waalikwa  mbalimbali waliohudhuria (hawapo pichani) kwenye hafla hiyo fupi ya kukabidhi msaada wa vifaa mbalimbali, iliyofanyika mapema leo asubuhi, ambapo Dunia ilikuwa ikitimiza idadi ya watu bilioni 7.
Mgeni rasmi pichani kati akiwa na wenyeji wake wakielekea kwenye wodi ya akina mama wazazi,kwa minajili ya kutoa msaada kwa wazazi saba waliojifungua watoto,ambapo dunia ilikuwa ikitimiza idadi ya watu bilioni 7.
Mgeni rasmi, muwakilishi wa shirika la mfuko wa idadi ya watu la Umoja wa Mataifa (UNFPA)-Tanzania,Dr Julitta Onabanjo akiwa amebeba mtoto kuonyesha ishara ya kuongezekwa wa watu duniani  na kufikia bilioni 7 mapema leo asubuhi katika hospitali ya TMK jijini Dar es Salaam.

Dr.Julitta Onabanjo akiwapa pole na hongera kwa akina mama wazazi waliojifungua usiku wa kuamkia leo,kwenye hospitali ya Temeke, ambapo Dunia ilikuwa inatimiza idadi ya Watu bilioni 7.
Mgeni rasmi,ambaye pia ni muwakilishi wa shirika la mfuko wa idadi ya watu la Umoja wa Mataifa (UNFPA)-Tanzania,Dr Julitta Onabanjo akiwa ameambatana na wenyeji wake wakiwa kwenye wodi ya Wanawake kwa ajili ya kutoa misaada kwa akina mama saba walijifungua usiku wa kuamkia leo,ambapo Dunia ilikuwa inatimiza idadi ya watu bilioni saba,na Tanzania ilikuwa inatimiza idadi ya watu bilioni 44.
Pichani shoto ni Muwakilishi wa shirika la mfuko wa idadi ya watu la Umoja wa Mataifa (UNFPA)-Tanzania, Dr . Julitta Onabanjo akiwa amembeba mtoto aliyezaliwa usiku wa kuamkia leo,kwenye hospitali ya Wilaya ya Temeke, jijini Dar es Salaam, ambapo Dunia ilikuwa inatimiza idadi ya watu Billioni 7, anayetazama pichani kulia na Mama wa Mtoto huyo aliyejitambulisha kwa jina la Kulwa Juma. 
Dr . Julitta Onabanjo akiwa na akina mama 7 waliojifungua usiku wa kuamkia leo, ambapo kupitia shirika la mfuko wa idadi ya watu la Umoja wa Mataifa (UNFPA)-Tanzania lilitoa msaada wa vitu mbalimbali kwa akina mama hao ikiwemo pia hospitali  hiyo kwa kupatiwa vifaa mbalimbali vya watoto.
Wafanyakazi wa shirika la mfuko wa idadi ya watu la Umoja wa Mataifa (UNFPA)-Tanzania wakijadiliana jambo.
Mgeni rasmi, muwakilishi wa shirika la mfuko wa idadi ya watu la Umoja wa Mataifa (UNFPA)-Tanzania,Dr Julitta Onabanjo akikabdhi sehemu ya msaada wa vifaa mbalimbali vilivyotolewa na shirika hilo kwa Mganga mkuu wa Manispaa ya Temeke, Dr. Sylvia Mamkwe, mapema leo asubuhi kwa ajili ya hospitali hiyo
Mgeni rasmi, muwakilishi wa shirika la mfuko wa idadi ya watu la Umoja wa Mataifa (UNFPA)-Tanzania,Dr Julitta Onabanjo akikabdhi sehemu ya msaada wa vifaa mbalimbali vilivyotolewa na shirika hilo kwa Mganga mkuu wa Manispaa ya Temeke, Dr. Sylvia Mamkwe, mapema leo asubuhi kwa ajili ya hospitali hiyo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: