MBUNGE wa jimbo la Morogoro Kusini Innocent Kalogeles amesema kuwa ili kupata suluhisho sahihi la migogoro ya wakulima na wafugaji ni lazama viongozi wa vijiji kutekeleza agizo la kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Morogoro la kuhakiki upya idadi ya mifugo iliyopo katika wilaya hiyo.

Akizungumza na mwandishi katika mahojiano maalum jimboni humo, mbunge huyo alisisitiza kuwa sambamba na kuhakiki idadi ya mifugo iko haja ya kuwachukulia hatua wafugaji wanaoingia kinyemela pasipo ruhusa za vijiji husuka ikiwa ni pamoja na kuwafukuza kutoka katika wilaya hiyo.

Kaligelis alieleza kuwa lengo la kamati ya ulinzi na usalama la kuzitaka serikali za vijijini kufanya uhakiki wa wafugaji na mifugo yao ni zuri kwani litasaidia kuwabaini wafugaji ambao waliingia katika kijiji kinyume na utaratibu.

Alisema kujitokeza kwa migogoro hiyo kunadaiwa kuwa ni uzembe wa baadhi ya ya viongozi wachache wa vijiji walioruhusu mifugo mingi kuliko kiasi kuingia katika vijiji vyao hali ambayo alidai kuwa kumesababisha ardhi kutokidhi idadi kubwa ya mifugo iliyoingia.

“Migogoro hii kwa kiasi kikubwa imechangiwa na utendaji mbuvu wa viongozi kuanzia ngazi ya kijiji hadi tarafa ambao watendaji wamekuwa wakidaiwa kushiriki kuruhusu mifugo kuingia na hivyo ardhi kuonekana kuwa ni ndogo kutokana na uwingi wa mifugo inayozaliana kila mwaka,” alisema Kalogeles.

Kalogeles alisema kuwa mifugo imekuwa mingi ikilinganishwa na ardhi ambayo hivi sasa inaonekana kuwa ni ndogo na kwamba likifanyika zoezi hilo la uhakiki wa mifugo na kuwarejesha makwao wafugaji walioingiza mifugo kinyemela itakuwa suluhisho la kudumu katika wilaya hiyo.

Hivi karibuni katika kitongoji cha Lukoni kijiji cha Kongwa tarafa ya Mvuha mkoani Morogoro kulitokea mgogoro wa wakulima wa kabila wa wakutu na wafugaji wa jamii ya kisukuma baada ya wakulima wa kijiji cha Kongwa kuchoma moto nyumba za wafugaji zaidi ya saba na kuharibu mali mbalimbali ikiwemo chakula.

Zaidi ya kaya saba zilipoteza makazi katika sakata hilo lililoibuka kutokana na madai ya wafugaji kuingiza mifugo katika mashamba yenye mazao kisha kulisha na kuwapiga sambamba na kuwajeruhi wakulima wakati wakijaribu kuondoa mifugo ili wasiharibu mazao yao.

Kutokana na tukio hilo mbunge wa jimbo la Morogoro Kusini Innocent Kalogeles Septemba 3 mwaka huu alifika katika kijiji cha Kongwa kwa lengo la kusuluhisha mgogoro huo ambao hivi sasa unanekana kutulia huku wakulima wakisubiri maamuzi ya serikali ya wilaya hiyo juu ya kuwachukulia hatua ya wafugaji walioingia kinyume na taratibu ambao wana kesi za kuingiza mifugo katika mashamba yao na kulisha mazao zilizofunguliwa ofisi ya tarafa Mvuha na kituo kidogo cha polisi Mtombozi-Matombo ili kulipwa fidia.

Katika ofisi ya tarafa na kituo kidogo cha polisi Mtombozi-Matombo kuna zaidi ya kesi 20 zilizofunguliwa kwa madai ya wafugaji wa jamii ya kisukuma kudaiwa kulisha mazao katika mashamba ya wakulima wa kijiji cha Kongwa katika tarafa hiyo ya Mvuha.

Uchunguzi wa kina uliofanywa na mwandishi watu juu ya mgogoro huo ambaye alifika katika kijiji cha Kongwa na kitongoji cha Lukoni umebaini kuwa ipo haja ya kutatua mgogoro huo haraka vinginevyo kunaweza kutokea maafa kama yaliyotokea wilaya ya Kilosa zaidi ya miaka minee iliyopita mkoani hapa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: