Wazoa takataka wakikusanya taka na kuweka kwenye gari bila ya kuwa na vifaa ya kujikinga na magonjwa eneo la Mombasa jijini Dar es Salaam.
Ujenzi unaendelea katika barabara ya Pugu jijini Dar es Salaam.
Vijana ambao wameamua kujiajili kwa kukusanya makopo ya maji kwa ajili ya kuyauza kiwandani. Ambapo kilo moja huuzwa kwa tsh.300/=
“Asilimia kubwa sana ya wananchi wa nchi ya Tanzania wanatumia nishati ya kuni na mkaa kwa kupikia. Ni dhahiri kabisa ukataji wa miti ili kukidhi haja hiyo ni mkubwa kila mwaka. Bila ya kuwa makini kwa suala hilo la nishati mbadala ya kupikia badala ya mkaa au kuni, uhifadhi wa mazingira kwa kutokata miti utakuwa ni ndoto.” Hiyo ni hali halisi ya wakazi wa Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam ambao wanafanya biashara ya mkaa. Ni vyema serikali na wanaharakati wakachukua mkondo wake kukomesha hali hii.
Toa Maoni Yako:
0 comments: