Msanii wa bendi ya Machozi, Mwinyi akiburudisha mduara mida ya saa nane kasoro wakati tukio hili la kusikitisha lilipotokea.
---
Nazungumza kwa masikitiko sana nikiwa kama mmoja ya waathirika wa jambo hili ambalo limetokea usiku wa leo Nyumbani Lounge jijini Dar es Salaam.
Ilikuwa ni majira ya saa nane kasoro usiku leo wakati bendi ya Machozi ikiburudisha ndani ya Nyumbani Lounge jijini Dar es Salaam ndipo ilipotokea hali ambayo watu wengi hawakuielewa ila wachache ndiyo waliweza kutambua kilichotokea, nilishtuka kuona watu wanatoka ndani wakikimbilia nje huku wakikohoa, wakipiga chafya na kulalamika kifua kubana na koo kuwasha... ndipo muda mfupi baada ya watu kuwa wametoka nje iligundulika kumbe kuna mtu amepulizia sumu kwa lengo la kuharibu onyesho hilo.
Baada ya kuwa watu wametoka nje, milango yote ilifunguliwa na hewa chafu ilitoka nje na watu kuendelea na Burudani kama kawaida.
Kajunason Blog inawapa pole watu wote waliopatwa na mkasa huu na tunakemea kitendo hicho cha kinyama kwa mtu aliyefanya. Pia tunatakiwa kuheshimu biashara za watu na kuacha roho mbaya ambayo imekuwa ikirudisha maendeleo ya watu nyuma ikiwemo ndugu zako wewe ambaye umefanya kitendo hicho.

Toa Maoni Yako:
0 comments: