Shindano la kumsaka mrembo wa Chuo
Kikuu cha Kampala International University 2011 litarajiwa kufanyika
jumamosi hii katika ukumbi wa Savanna Lounge (Quality Center) uliopo
barabara ya Pugu, jumla ya warembo 12 wamejitokeza kuwania taji hilo siku
ya tarehe 22 oktoba mwaka huu.
Shindano litapambwa na wasanii wa
kizazi kipya kipya Dully Sykes, D-nob, Ngoma za asili na vijana wa
kutikisika (Shers), mbali ya burudani hizo kutakuwa na suprise ya majaji
pamoja masupastaa wa movie.
Miss Kampala Internationa 2011
imeandaliwa na serikali ya wanafunzi ikishirikana na wadau maarufu wa
mambo ya urembo na mitindo nchini Tanzania, tiketi za fainali hizi
zinapatikana CLOUDS FM, CHUONI KWAO, JB BELMONT HOTEL, SAVANNA
LOUNGE (Quality Center) Kitchen Hut (Nlimani City) kwa kiasi cha 10,000/=
(Regular) na V.I.P 30,000/=
Shindano hili limedhaniwa na Savanna Lounge hotel, Bel mont hotel, Clouds Fm na Air Uganda.
Toa Maoni Yako:
0 comments: