Mwakilishi wa Tigo Alpha Akimu ambaye ni meneja mauzo wa Tigo kwa mikoa ya Kigoma na Kagera akiongea na wanafunzi mara baada ya kukamilisha hafla ya kuwapa vitabu wanafunzi vilivyoghalimu zaidi ya shilingi milioni tano kupitia kampeni inayoendeshwa na Tigo iitwayo Tigo Tuchange..
Meneja wa mauzo kwa mikoa ya kigoma na Kagera Alpha Akimu akikabidhi vitabu kwa katibu tawala wa manispaa ya Bukoba Agnes Alex kwa niaba ya shule ya msingi Rwamishenye wakati wa hafla ya kukabidhi vitabu 1022 vilivyotolewa na tigo kupitia kampeni yake ya Tigo tuchange.
Mwakilishi wa Tigo Alpha Akimu ambaye ni meneja mauzo wa Tigo kwa mikoa ya Kigoma na Kagera akiongea na wanafunzi mara baada ya kukamilisha hafla ya kuwapa vitabu wanafunzi vilivyoghalimu zaidi ya shilingi milioni tano kupitia kampeni inayoendeshwa na Tigo iitwayo Tigo Tuchange.
---
Kampuni ya simu za mikononi ya tigo imekabidhi vitabu kwa shule ya msingi Rwemishenye iliyopo wilayani Bukoba mkoani Kagera kupitia kampeni yake ya “Tigo tuChange” ikiwa ni moja ya jitihada za kampuni hii katika kuchangia elimu.

Mwezi iliopita Tigo ilitoa vitabu kwa shule za msingi za msingi  Nyasa1 iliyopo wilayani Nzega mkoani Tabora na Tuangoma ya jijini DSM  hivyo hii leo shule ya msingi Rwemishenye iliyopokea vitabu hivi imekuwa ya tatu tangu kuazishwa kwa kampeni  ya Tigo tuChange na kampeni hii itaendelea kwa mikoa ya Singida na Mtwara.

Akielezea madhumuni ya kampeni ya Tigo Tuchange wakati wa kukabidhi vitabu katika shule hiyo, Meneja mauzo wa Tigo kanda ya kigoma na Kagera Alpha Akimu amesema Tigo ni sehemu ya jamii na kwa jamii yoyote ili iweze kuendelea elimu iliyobora ni nguzo muhimu na kwa kutambua hilo ndio maana tigo imeamua kuchangia elimu kupitia vitabu.

Alpha ameongeza kuwa uzalendo wa watanzania na hasa katika kuipenda Tigo umetoa msukumo wa wao kurudisha sehemu ya faida kwa jamii, ‘watanzania wameendelea kuwa msaada mkubwa kwetu na meendelea kutuunga mkono siku zote sasa na sisi kwanamna ya pekee hasa ukizingatia kuwa Tigo ni sehemu ya watanzania hatuna budi kurudisha sehemu ya kile tunachokipata kwa jamii inayotuunga mkono siku zote.

Akiongea kwa niaba ya mkurugenzi wa manispaa ya Bukoba,  Afisa elimu wa manispaa ya Bukoba Baganda Elpidius amesema anafurahia jitihada mbalimbali zinazofanywa na Tigo katika kusaidia sekta ya elimu. ‘Hatua hii ni nzuri na yenye manufaa kwa Taifa kwani vitabu vimeendelea kuwa tatizo kubwa katika sehemu mbalmbali ndani ya nchi na ukweli ni kwamba ili uweze kugundua matatizo yanayozikumba jamii hasa katika elimu pita katika ofisi zetu kwani mahitaji ni makubwa na serikali inajitahidi kuhakikisha matatizo haya yanaondoka lakini mchango wa wadau katika kufanikisha hili unahitajika kwa kiasi kikubwa hivyo tunaishukuru Tigo kwa hatua hii iliyoanzisha ambayo itakuwa mfano mzuri na wa kuigwa na makampuni mengine binafsi”

Kampeni hii ya Tigo tuChange inatokana na fedha zilizopatikana kupitia programu maalumu  iliyoandaliwa na Tigo tarehe 09 mwezi wa saba 2011 ambapo kuanzia saa tatu mpaka mpaka saa nne  mteja aliyenunua muda wa maongezi kuanzia shilingi mia tano na kuendelea fedha hiyo ilipeleckwa katika kampeni hiyo na jumla ya shilimgi  25,930,160 zilikusanywa ambazo ndizo zilizotumika kununulia vitabu.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: