Ni Bush Star Search: Ndani ya kijiji cha Bujora kulikuwa na Mwanadada maarufu anayetikisa na kusumbua katika sanaa za aina zote iwe ni ngoma, maigizo, kuimba, sarakasi alikuwa juu sana hata wanakijiji walikuwa wakimwaminia. Ukaguzi wa Bush Star Search ulipotia timu kijijini Bujora kutafuta vipaji mwanadada huyo alionyesha kila aina ya kipaji alichokuwanacho lakini laaa!! Majaji wakamtosa!

-OOh Mie najuwa kuimba – Akaimba Hola huna kipaji!!
-Mie najuwa kucheza - Akacheza ngoma Hola huna kipaji!!!!!
-Akafanya Manjonjo yote ….Huna kipaji!!!!!

Mwisho wa siku majaji wakamwambia “dada ungeondoka tu mahala hapa, huna kipaji cha sanaa aina yoyote ile na hata katika wale kumi tunaowahitaji HAUMO!”

Dada akauliza “sasa nyie mnataka nini kwani kama ni sanaaa uliza watu wote wananifahamu hapa kijijini?” na mshindi wa kwanza kiongozi yaani Chief alitenga ng’ombe 12 kama asili ya watu kabila la Sukuma hivyo washiriki wote wakajishughulisha kutwaa zawadi hiyo.

Dada alipokataliwa akaweka kinyongo na kwenda kushtaki kwa bibi yake ambaye alikuwa mtaalam wa kucheza na vibuyu. Bibi akamwambia omba mizimu utakalo, Dada akaiomba mizimu….

Siku wale Top Ten wanaondoka dada akawaambia majaji “Kama nyie ni wajanja basi tuone kama mjini mtafika….." HAPO NDIPO SHESHE NA BALAAA LINAPOANZA.... ISUBIRI MUVI INAITWA 'BUJORA'
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: