Mtoto Cecilia alitangazwa hivi karibuni na Vituo mbali mbali vya habari akiomba msaada wa kusaidiwa pesa za matibabu ambazo zingeweza kumwezesha kufanyiwa operesheni ya moyo ambao umempelekea mpaka Tumbo lake kuvimba kama unavyoliona.
Taarifa za Cecilia ziliweza kutolewa na Miss Tanzania wa mwaka 2006 Bi. Hoyce Temu pale alipoamua kujitokeza na kumtangaza Cecilia akiomba msaada huo. Wasamaria wema walijitokeza na kumsaidia Cecilia mpaka akaweza kwenda India kwa matibabu, cha kusikitisha sana ni kwamba matibabu yake kwa njia ya operesheni yameshindikana kutokana na moyo wake kwa upande mmoja kuathirika na sumu ambayo madaktari wa India wamesema inasababishwa na Sumu ambayo ipo kwenye Mihogo, sumu hiyo huwaathiri sana watoto wenye umri kama wake.
Kwa hiyo imekuwa ni vigumu kumfanyia operesheni hiyo, wakashauri atumie dawa tu ili kuweza kuitoa sumu hiyo, Mtoto Cecilia mpaka sasa hali yake sio nzuri anawaomba watanzania mumuombee ili aweze kupona na aweze kutimiza azma yake ya kuwa Mwalimu. Watanzania tunashauriwa tukiona hali ambayo ni tofauti kwa watoto wetu tuwawaishe Hospitali mapemakwa uchunguzi tunaweza tukawahepusha na hali kama hii aliyofikia Cecilia.
Toa Maoni Yako:
0 comments: