Basi la Shabco Express ambalo lilikuwa likieleka Arusha leo limepata ajali
mbaya ya kupinduka katika kona za Msambizi, Korogwe. Kwa mujibu wa abiria hao
walisema kuwa gari hilo
lilipata ajali hiyo baada ya kulikwepa gari dogo na kujikuta likitumbukia mtaloni
kutoka na hali ya mvua na ukungu uliokuwa umeenea barabara nzima. Hakuna mtu aliyekufa katika ajali hiyo
Abiria wakiwa wanaangalia ustarabu wa kusubiri gari lingine ili waendelee na safari yao, hapo ilikuwa ni majira ya saa tisa mchana huku mvua ikinyesha.
Abiria wakinyeshewa huku wakiwa na watoto wadogo mgongoni.
Gari hilo likionekana kwa upande wa nyuma.
Toa Maoni Yako:
0 comments: