FAINALI ya shindano la kumsaka mkali wa kuimba la Bongo Star Search ‘Second Chance’ 2011, inatarajiwa kuchukua nafasi Oktoba 14, mwaka huu (Ijumaa), ndani ya Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na mtandao huu mapema leo, mkurugenzi wa BSS, Rita Paulsen ‘Madam’ alisema kuwa fainali hiyo itatumbuizwa na msanii mkubwa kutoka nchini Nigeria, Chinedu Okoli N’Abania ‘Mr Flavour’ anayetamba na wimbo wa Ashawo.
Alisema mbali na Mr Flavour, washiriki waliowahi kutikisa kwenye shindano hilo miaka ya nyuma kama Peter Msechu, Jumanne Iddi, Misoji Nkwabi, Mariam Mohamed na Leah Muddy nao watamwaga burudani ya kihistoria.
Aliweka wazi kuwa, pia washiriki walioingia kwenye nne bora mwaka huu watapamba usiku huo ikiwa pamoja na kuchuana hadi atakapopatikana mshindi wa shindano hilo.
Alisema zawadi kwa mshindi itakuwa Sh. milioni 40, Sh. milioni 10 kwa mshindi wa pili na Sh. milioni 5 kwa mshindi wa tatu.
Viingilio vya shoo hiyo ni Sh. 20,000 kwa viti vya kawaidi, elfu 50,000 kwa VIP na 100,000 kwa VVIP ambapo watakaolipia VVIP watapata vinywaji vyote bure.
Tiketi zitapatikana kuanzia tarehe 11 katika maduka ya Shee Illussion Mlimani City na Millenium Towers Kijitonyama, Biggy Respect Kariakoo, Steers City Centre, katika maduka yote ya Zizzou Fashion, Beauty Point Shoppers Plaza, Mbalamwezi Beach Club Mikocheni kwa Walioba, Manywele Cosmetics Kinondoni, Best Bite, Engine Mbezi Beach na katika Ukumbi wa Diamond Jubilee .

Toa Maoni Yako:
0 comments: