Moja ya power Tillers aina ya VST SHAKTI MITSUBISHI zilizotolewa kwa washindi wawili waliopatikana katika promotionya kilimo kwanza iliyoandaliwa Tigo kwa kushirikiana na Noble Motors.
Bw. Max Mhagama ambaye ni meneja masoko na Mauzo wa kampuni ya NOBLE MOTORS akielezea ubora wa aina ya Power Tillers za VST SHAKTI MITSUBISHI zilizotolewa kwa washindi wawili waliopatikana leo jijini Dar es Salaam.
Mchambuzi wa Biashara (Business Analyst) wa Tigo David Mugittu akielezea jinsi promoshen ya KILIMO KWANZA YA TIGO ilivyoendeshwa  mara baada ya kuwapata washindi wa promosheni hiyo katika ofisi za kampuni ya Noble Motors jijini Dar es Salaam.
---
Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo leo imeendesha zoezi la kuwapata na kuwatangaza washindi wa jumla wa promosheni ya KILIMO KWANZA NA TIGO ambao wameshinda tractor aina ya Power tiller ikiwa ni moja kati ya mikakati ya kampuni hii katika kuiendeleza sera ya serikali ya kilimo kwanza.

Promosheni hii iliyoendeshwa na Tigo kwa kushirikiana na Noble Motors kwa miezi miwili, yaani tokea tarehe 16 August 2011 na kuishia tarehe 16 oktober 2011, ililenga kuwapata washindi wawili ambao ni wateja wa Tigo na wanaotumia huduma za MIA ZAIDI, TANO ZAIDI na HAMISHA SALIO na washindi hawa watapata power tillers mbili aina ya VST SHAKTI MITSUBISHI ambazo zimekwishasajiliwa na kulipiwa ushuru na gharama zote za usajili.

Mshiriki wa promosheni hii alitakiwa kutuma neno MIA ZAIDI kwenda number 15313 ambapo alipewa nafasi ya kutuma ujumbe 100 pamoja na muda wa maongezi wa dakika tano wa kupiga simu tigo kwenda tigo. Na mteja aliweza kujiongezea nafasi ya kushinda kwa kujiunga kila siku.

Pia mteja aliweza kushiriki kwa kujiunga huduma ya TANO ZAIDI ambapo mteja alitakiwa kutuma neno TANO ZAIDI kwenda namba 15313 na kupokea meseji 15 na dakika 2 za muda wa maongezi kila siku kwa mwezi mzima.

Njia ya tatu ya ushiriki ilikua ni kwa kugawana salio. Mteja alijipatia tiketi ya kushiriki droo kwa kuwagawia salio awapendao kwa kupiga *101*NAMBA YA AMTUMIAE*KIASI# halafu kubonyeza kitufe cha kupiga.

Mshindi wa kwanza alikuwa Macrine Charles wa Dar es Salaam, ni mwanafunzi na ana miaka 22. Mshindi wa pili anaitwa Edgard wa Dar Es Salaam ambayo ni mwanafunza wa chuo chaa ardhi.

Akiongea mara baada ya kuwapata washindi wa promosheni hiyo  Mchambuzi wa Biashara (Business Analyst) wa Tigo Bw. David Mugittu amesema kuwa hii ni uthibitisho tosha kuwa ahadi za kampuni ya simu ya tigo kwa wananchi ni za kweli, “Sisi Tigo tumekuwa tukifanya promosheni na kampeni mbalimbali lengo kubwa likuwa ni kuwajulisha waTanzania juu ya huduma nyingi zaidi tunazozibuni kwa lengo la kuwarahisishia maisha lakini kubwa zaidi ni kurudisha sehemu ya faida kwa jamii inayotujali siku zote”

Bw. Mugittu ameongeza pia kwa kusema “naamini kuwa washindi hawa watakuwa chachu kwa watanzania wengine ambao wapo katika sehemu mbalimbali nchini kushiriki katika promosheni hizi kwani ni faida siku zote na hakuna hatua ambayo utapoteza fedha unaposhiriki promosheni za Tigo kwani ile hela utayoipata itakupa huduma husika na pia kukuingiza katika kapu la ushindi, kumuinua mwananchi hasa wa kipato cha chini ni moja kati ya vipaumbele vyetu”. 

Akimalizia, .Mugittu aliwakumbusha wateja wa Tigo kuendelea kufurahia huduma za Tigo kwa KUONGEA BURE USIKU KUCHA baada ya dakika ya tatu saa nne usiku mpaka saa moja asubuhi.

Naye Max Mhagama ambaye ni meneja masoko na Mauzo wa kampuni ya NOBLE MOTORS amesema aina ya power Tillers hizi za VST SHAKTI MITSUBISHI zilizotolewa kwa washindi ni zile ambazo zimeonekana kuwafaa watanzania kwa kiasi kikubwa, ikizingatiwa kwamba zinao pia mfumo wa kuchabanga (rotary attachment) ambao umeunganishwa moja kwa moja hivyo kufaa sana katika mashamba ya mpunga. 

Power Tiller hizi zimekuwa zikifanya kazi kwa ufanisi mkubwa tangu mwaka 2006 ikiwa ni pamoja na kuthibitishwa na CAMARTEC ambacho ni chombo cha serikali kilichoandaliwa kwa ajili ya kuchunguza ubora na uwezo wa matrekta haya katika ardhi ya Tanzania. Pia ufanisi wa Power tiller hizi unaonekana katika uwezo wa ubebaji mzigo kutokana na uwezo wa trailer kuwa tani 1.5.

Bw. Max aliongeza kuwa “Pamoja na kufanya kazi kwa zaidi ya miaka mitano nchini Tanzania, sisi huwa tunatoa mafunzo jinsi ya kuendesha na kufanya ukaguzi wa matrector haya kwa wakulima, na tunatilia mkazo zaidi kwa yule mtu ambaye atakuwa analitumia shambani, kwa hiyo hata hawa washindi waliopatikana leo watapatiwa mafunzo kabla ya kuanza kuyatumia matrekta haya”
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: