Mwanamuziki Diamond (katikati) akipena mikono na Dk. Mdoe wakati wa zoezi la kutoa misaada Hospitali ya Ligula.  Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Safari Radio Foundation, Haroun Maarifa.  Wengine ni wafanyakazi wa hospitali hiyo.
---
Na Sijawa Omary, Mtwara

MSANII anayetamba katika muziki wa kizazi kipya (Bongo Flava), Naseeb Abdul ‘Diamond’,  ametoa misaada mbalimbali yenye thamani ya sh. 3,500,000 na laki tano katika wodi ya wazazi ya  Hospitali ya Ligula Mkoa Mtwara.

Akikabidhi msaada huo, Diamond alisema  yeye kama msanii amevutiwa kutoa msaada katika wodi ya wazazi kwa kuwa watoto wanaozaliwa watakuwa mashabiki wake na watapenda kazi zake hapo baadaye.  Msaada msaada huo umefadhiliwa na Safari Radio Foundation.

Alisema pia hufanya hivyo ni kuwa karibu na jamii katika kujenga upendo na mshikamano ili kupata ushauri ambao utakuwa tija katika utendaji wa kazi zake  kwani yeye pekee hawezi kupanga jambo pasipo kupata mwongozo kutoka kwa wadau wake.

“Wazazi ni watu wa kuwaheshimu na kuwaenzi  kwani kazi wanazotufanyia ni kubwa na nzito katika hatua zote hadi kufikia hapa tulipo,” alisema.
Aidha aliushukuru uongozi wa Safari Radio Foundation kwa kumpa fursa hiyo ya pekee kwani amepata faraja na heshima kubwa katika jamii sambamba na mashabiki wake kwa jumla.

Naye Mkurugenzi wa Safari Radio Foundation  ambaye pia ni Mkurugenzi wa Safari Radio FM, Haroun Maarifa,  alisema  taasisi yake imelenga katika kudumisha umoja na mshikamano.
Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk. Mdoe Mhuza, ameushukuru uongozi huo kwa msaada uliotolewa ambapo umeonyesha moyo wa kusaidia wagonjwa.

Mhuza aliwataka watu wengine kuiga mfano huo kwani siyo lazima kuitegemea serikali kwa kila kitu, na kwamba kutoa ni moyo siyo utajiri.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: