JESHI la Polisi Kitengo cha Usalama Barabarani, limewaonya madereva wanaotumia simu wanapoendesha vyombo hivyo, kwani wanachochea ongezeko la ajali.

Onyo hilo lilitolewa na Kamanda Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Ahmed Mpinga, alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu kuongezeka kwa matukio ya ajali za barabarani.

Alisema ajali zilizotokea kati ya Januari hadi Juni mwaka huu ni 12,124, ambazo zimesababisha vifo 1,764 na majeruhi 10,122.

“Ajali zilizosababisha vifo 1,475 na majeruhi 5892 na zile za kawaida zilikuwa 4789. Idadi hii ni jumla ya mikoa yote nchini.

“Nakiri kuwa kuna tatizo la upungufu wa askari wa kitengo cha uokoaji pindi ajali itokeapo. Lakini kupitia mikakati endelevu tuliyoiandaa, tunatarajia mwaka 2020 kupunguza idadi ya vifo sanjari na majeruhi,” alisema.

Aidha, Kamanda Mpinga alisema kutokana na hali hiyo, kwa siku watu 300,000 duniani hupoteza maisha kutokana na ajali za barabarani na kwa mwaka hukadiriwa kuwa watu milioni 1.3.

Mpinga alisema mbali na ajali hizo, jeshi hilo kwa kushirikiana na Radio One, wamezindua kampeni ya matumizi sahihi  ya barabara kwa wananchi wote.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: