Baadhi ya wanajeshi wa vikosi mbali mbali vya ulinzi wakibeba majeruhi Marium Mohamed Muradi (29) kutoka Tanga, aliyenusurika na kifo katika ajali ya kuzama kwa Meli ya Mv Spice Islander, katika ufukwe wa bahari ya Nungwi Mkoa wa kaskazini Unguja usiku wa kuamkia leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa na Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad wakiwa ni wenye huzuni sana wakati walifika eneo la tukio la ajali ya meli ya Spice Islander, iliyozama katika bahari ya Nungwi mkoa wa kaskazini Unguja.
Baadhi ya wanajeshi wa vikosi mbali mbali vya ulinzi wakibeba majeruhi walionusurika na kifo katika ajali ya kuzama kwa Meli ya Mv Spice Islander, katika ufukwe wa bahari ya Nungwi Mkoa wa kaskazini Unguja usiku wa kuamkia leo.
Watu waliojazana kuanzia uwanja wa maisara hadi hospitali
kuu ya mnazi mmoja wakisubiri kuwatambua maiti zao,karibu matayarisho yote
yanayo staiki kufanyiwa maiti yamekamilika kinachosubiliwa ni upokeaji wa
maiti, tayari watu wasiopungua 300 wameokolewa wakiwa wazima wengi wao ni
watoto na kinamama.
Balozi Seif Ali Iddi akitoa maelekezo juu ya utaratiwa wa
kufuatwa kwa watu watakaokuja kuangalia maiti zao ndani ya hema, hadi muda huu
tayari maiti mbili zimesha hifadhiwa ndani ya hema hilo tayari kwa kutambuliwa
katika maandalizi hayo idara ya maafa wakishirikiana na Ofisi ya Mufti wa Zanzibar
watazihudumia maiti zote kwa kuzikosha,kuzivika sanda na kuzika.
Toa Maoni Yako:
0 comments: