Na Pardon Mbwate wa Jeshi la Polisi, Kigoma
Baiskeri zirizotumika kusafirishia risasi 2200 kushoto ni RCO Joseph Konyo katikati ni RPC Frasser Kashai ariefuata OC CID Moha
 Jeshi la polisi mkoa wa kigoma limeendelea kufanya misako endelevu dhidi ya makosa mbalimbali ya jinai yakiwemo unyang’anyi wa kutumia silaha, wahamiaji haramu, madawa ya kulevya na makosa ya usalama barabarani. aidha mbinu mbalimbali zimetumika katika kuleta mafanikio ikiwemo doria, kufanya misako mbalimbali na vizuizi vya barabarani.   mafanikio yaliyopatikana ni kama ifuatavyo :-

SEPT 10 2011 Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma ACP Fraisser Kashai, amesema kuwa jeshi la polisi limefanikiwa kukamata Risasi 2200  mnamo tarehe 07/09/2011 majira ya saa 01:00hrs huko uvinza katika wilaya na mkoa wa kigoma. askari polisi wakiwa kazini  katika kizuizi cha barabarani (beria) waliwasimamisha watu watano waliokuwa na baiskeli kila mmoja kwa nia ya kuwapekua baada ya kuwatilia mashaka.
ACP FRASSER KASHAI RPC
 Kamanda Kashai amesema kuwa baada ya kuwatilia muda waliokuwa wakisafiri kwa baiskeli ghafla watu hao baada ya kugundua kuwa walikuwa wamesimamishwa na askari walitupa baiskeli zao na kukimbia huku wakizitelekeza baiskeli zao. vifurushi vilivyokuwa  katika baiskeli hizo vilipekuliwa na zilipatikana risasi 2200 za bunduki za kivita aina ya S.M.G. / S.A.R

Aidha Kamanda amesema kuwa Polisi waligundua risasi  hizo zilikuwa zikisafirishwa kwa nia ya kufanyia vitendo vya uhalifu ndani na nje ya mkoa wa kigoma. jeshi la polisi linaendelea na msako mkali dhidi ya watuhumiwa hao waliotoroka.
SSP JOSEPH KONYO RCO
Aidha Kamanda amesema jumla ya tshs 740,000/= zilikusanywa kama faini za  makosa mbalimbali ya usalama barabarani yaliyokamatwa katika operesheni maalumu iliyofanyika kati ya tarehe 08/09/2011 na 09/09/2011.

Hata hivyo Kamanda Kashai amesema kuwaJeshi Jeshi la polisi linatoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano katika kufanikisha vita ya  kupambana na uhalifu na wahalifu

Sanjari na hilo madereva na wamiliki wa vyombo vya usafiri wanatakiwa kufuata sheria na kuhakikisha magari yao yako katika viwango vya kubeba abiria kwa mujibu wa sheria na kwa mara nyingine ninawaimiza madereva wote ambao reseni zao zimekwisha muda wake kwenda kwenye mamlaka husika na kupata leseni hizo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: