Timu ya Yanga Africans ya Tanzania imechukua ubingwa wa michuano ya klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati baada ya kuichapa Simba Sports club pia ya Tanzania kwa goli 1-0.

Mbali na kuchukua kombe, Yanga pia itazawadia dola elfu 30 za Kimarekani.

Bao hilo la pekee na la ushindi limefungwa na Kenneth Asamoah, mchezaji wa kulipwa kutoka Ghana. Mara baada ya dakika tisini kumalizika kwa timu hizo kutoka suluhu ya bila kufungana, dakika 30 ziliongezwa na ndipo Goli hilo la ushindi kwa Yanga likapatikana nalo ni katika dakika ya 108.

Timu hiyo imekabidhiwa kombe lake kizani mara baada ya umeme kukatika nazo juhudi za kuurejesha umeme huo kushindikana.

Mchezo huo wa fainali umechezwa Uwanja mpya wa Taifa jijini Dar es salaam.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: