Pichani ni JCB katikati akiwa na washikaji zake kulia ni Daz Knowlege waliomsindikiza uwanja wa Kilimanjaro International Airport, Kilimanjaro. 
Msanii mkongwe katika muziki wa kizazi kipya hip hop JCB Makala (katikati) ameondoka jana nchini kwenda Denmark kwa ajili ya kwenda kufunga ndoa na mchumba wake ambaye yupo huko. Akizungumza na blog hii ya Kajunason Blog (Habari na Matukio) katika uwanja wa ndege wa Kilimanjaro International Airport uliopo Kilimanjaro jana ilipokutana nae uso kwa uso. JCB Malaka alisema kuwa anafurahi sana kwani alikuwa anasubiri kwa muda mrefu ili kuweza kutimiza hilo. JCB ni msanii mkongwe ambaye anafanya vyema katika muziki wa hip hop na makazi yake ni jijini Arusha.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: