---
MAANDALIZI Tamasha la 14 la kimataifa la filamu ZIFF Festival sasa yamekamilika ambapo linatarajiwa kuanza mwishoni mwa wiki hii.
Akizungumza jana katika mkutano na waandishi wa habari Profesa Martin Mhando amesema kwamba tamasha hilo la mwaka huu litakuwa la aina yake hasa kuzingatia uzoefu walionao tangu lilipoanazishwa.
Profesa Mhando alisema kuwa mwaka huu katika tamash hilo kutakuwa na mambo mengi ya kuvutia ikiwa ni pamoja na maonyesho ya wanamuziki wenye majina na wa Kimataifa kama Shaggy na Oliva Mutukudzi. Mbali ya wasanii hao pia filamu 71 zitaonyeshwa ikiwamo filamu za hapa nchini.
Muhando alisema kutakuwa na filamu za mataufa mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutoka nchi za Iran movie, Swahili Bongo day na filami nyingine kutoka katika nchi mbalimbali zitaonyeshwa.
Naye Meneja wa Bia ya Tusker ambao ni wadhamini wakuu wa Ziff Ritha Mchaki ametoa wito kwa mashabiki na wadau mbalimbali kujitokeza kwenye tamasha hilo.
Wadhamini wengine ni Kampuni ya kinywaji baridi ya Coca Cola. Wakati huohuo Mhando ameongeza kwakusema kuwa filamu 58 zitashindanishwa na zawadi mbalimbali zitatolewa.
Mwisho anamalizia kwa kusema kuwa katika tamasha hilo watatoa tuzo ya heshima kwa marehemu Hammie Rajab ambaye alikuwa mtengenezaji wa filamu mbobevu hapa nchini aliyefariki dunia Aprili 21 mwaka huu.
Mbali ya kuwa mtengenezaji wa filamu pia alikuwa mwandishi wa vitabu vya tamthilia pia aliwahi kufanya kazi mbalimbali za uandishi.
Chanzo www.bongoweekend.blogspot.com
Toa Maoni Yako:
0 comments: