Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeteua waamuzi kutoka Misri kuchezesha pambano la mkondo mmoja kati ya Simba ya Tanzania na Wydad Casablanca ya Morocco litakalofanyika Mei 28 mwaka huu Uwanja wa Petrosport jijini Cairo, Misri.

Mechi hiyo ya kutafuta timu ya kucheza hatua ya makundi ya Ligi ya MabingwaAfrika itaanza saa 12 kamili jioni kwa saa za Cairo.Waamuzi hao ni Farouk Mohamed atakayepuliza filimbi wakati wasaidizi wake niMohamed Waleed na Hassan Sherif. Mwamuzi wa mezani (fourth official) ni OmarFahim wakati Kamishna wa mchezo huo ni Magdy Shams El Din kutoka Sudan.

Mshindi atacheza kundi B pamoja na timu za Al Ahly ya Misri, Esperance ya Tunisia na Moloudia Club d’Alger ya Algeria.

Timu itakayoshindwa itaingia katika hatua ya 16 bora ya michuano ya Kombe la Shirikisho ambapo itacheza mechi yakwanza nyumbani dhidi ya Daring Club Motema Pembe ya DRC kati ya Juni 10, 11 na 12 mwaka huu.

Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),Muhsin Balhabou ndiye atakayeongoza msafara wa timu ya Simba kwenda Cairo kwaajili ya mechi hiyo.

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: